"Kajala alikosea kurudiana na Harmonize, wataachana! Ningekuwa mzazi ningempa laana" - Lokole

Juma Lokole alisema kila mudac walikuwa wanaongea na Kajala na alikuwa anamhakikishia hangerudiana na Harmonize.

Muhtasari

• “Kwangu mimi nilishtuka kwa sababu Kajala ni mtu ambaye nilikuwa naongea naye vitu vingi sana na alikuwa anaapa mpaka kwa miungu kwamba sitoweza kurudiana," - Lokole.

Juma Lokole
Juma Lokole
Image: Screenshot:YouTube

Mtangazaji na mdaku Juma Lokole hatimaye amerudi tena baada ya ukimya wa muda na kulizungumzia suala zima la Harmonize na Kajala kuvishana pete za uchumba.

Ikumbukwe mdaku huyo ndiye alikuwa mstari wa mbele kumsema vibaya Harmonize huku akiapa kwamba hakuna namna yoyote msanii huyo wangeweza kurudiana na Kajala.

Sasa anasema uhakika wa msimamo wake ulikuwa unatokana na kwamba alikuwa anazungumza na Kajala na mwanamama huyo kumhakikishia kwamba hawezi rudiana na Harmonize. Lokole alisema hata yeey alipigwa na butwaa baada ya kuona Kajala akirudiana na Harmonize tena.

“Kwangu mimi nilishtuka kwa sababu Kajala ni mtu ambaye nilikuwa naongea naye vitu vingi sana na alikuwa anaapa mpaka kwa miungu kwamba sitoweza kurudiana. Bado nasimamia pale pale kwamba ni akili mbovu na ufinyu wa kutoelewa maneno. Kwa hiyo niliumia kama binadamu, nilishtuka kama mtu wangu wa karibu,” Juma Lokole alijikosha.

Mtangazaji huyo anasema baada ya Kajala kukubali msamaha wa Harmonize, alidhalilika sana na kusema kwamba yeye angekuwa ndiye baba mzazi wa Kajala basi angempa laana, na kusema kwamba sasa wameshapotezeana na Kajala kwenye mitandao ya kijamii.

Alisema msimamo wake uko pale pale kwamba mahusiano yake na Harmonize hayawezi enda mahali na kwamba wataachana tu muda si mrefu.

“Ningempa laana na nguo ningemvulia kabisa asilimia mia kama ningekuwa mzazi wake. Hakuudhamini utu wake kadhamini pesa,” Juma Lokole alisema.