Otile: Video ghali ni collabo na Kizz Daniel, iligharimu 2.6M, haikufanya vizuri kwa mauzo

Otile Brown alisema maandalizi ya video hiyo kwa jumla iligharimu 2.6M, video yenyewe ikichukua 1.7M

Muhtasari

• Msanii huyo alidokeza kwamba alipata milioni yake moja taslimu mwaka 2017 baada ya kuachia kibao cha Mapenzi Hisia.

•Alisema kwa sasa yupo singo baada ya kutengana na mpenzi wake wa muda mrefu kutoka Etrhiopia, Nabayet.

• Otile Brown kwa sasa ndiye balozi mkuu wa kusukuma mauzo ya simu za Tecno Cammon kutoka kwa kampuni ya Tecno.

Msanii wa kizazi kipya Otile Brown katika mahojiano ndani ya rdio Jambo.
Msanii wa kizazi kipya Otile Brown katika mahojiano ndani ya rdio Jambo.
Image: Radio Jambo (Facebook)

Msanii maarufu wa kizazi kipya nchini Kenya Otile Brown amefichua kwamba wimbo ambao aliogharamika sana kuutoa ni ile collabo ya Baby Go aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria, Kizz Daniel. Ngoma ambayo mpaka sasa imekwama kwa watazamaji milioni 1.4 tu kwenye jukwaa la kusambaza miziki la YouTube.

Otile Brown akizungumza katika mahojiano ya moja kwa moja na mtangazaji Massawe Japanni kweney redio Jambo alisema kwamba licha ya kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwenye kutayarisha video hiyo, mapato hayakufana sana kwani nddio ngoma ambayo haijafanya vizuri vile zaidi ya mwaka mmoja baadae.

Mwanamuziki huyo alisema kwamba video hiyo ilimgharimu kiasi cha shilingi milioni 2.6 pesa taslimu za benki kuu ya Kenya, kiasi ambacho ni ghali zaidi katika safari yake ya muziki.

Alisema kwamba wasanii wa kutoka Nigeria ni ghali sana ukiwashirikisha katika mradi wa ngoma na kusema video yenyewe ilichukua kiasi cha shilingi milioni 1.7 na kiasi kilichosalia kilitumika kwenye maeneo ya kutengeneza video na mambo mengine.

Otile Brown alifichua kwamab milioni yake ya kwanza ile alipokezwa taslimu ilikuwa ni mwaka wa 2017 baada ya kuachia kibao moto kilichovuma kwa jina Mapenzi Hisia.

Kwa sasa msanii huyo ambaye hayuko katika mapenzi baada ya kuachana na aliyekuwa mchumba wake wa miaka mitatu, mtoto kutoka Ethiopia Nabayet, anajiandaa katika tamasha kubwa lilaloandaliwa na shirika la habari la Radio Africa kwa kushirikiana na benki ya Stanbic, tafrija inayoenda kwa jina Stanbic Yetu Festival itakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu katika ukumbi wa tafrija wa Carnivore jijini Nairobi

Wiki chache zilizopita aliteuliwa kama balozi wa kampuni ya simu ya Tecno ambapo atakuwa anapiga kazi kupandisha mauzo ya simu za Tecno Cammon.