logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Fahyvanny aingia ligi ya Pritty Vishy, atangaza kuongezeka kwa mahari yake

Fahyvanny ambaye ni mzazi mwenza wa msanii Rayvanny alitangaza kwamab mahari yake imeongezeka, aingia ligi ya pritty Vishy

image
na Radio Jambo

Habari18 July 2022 - 11:33

Muhtasari


• Mwanamitindo huyo alisema kwamba kutokana na uzuri wake, itabidi mahari iongezeke kwa mwanqaume yeyote mwenye mipango ya kupeleka posa.

Mwanamitindo na balozi wa brand mbalimbali Fahyvanny

Mwanamitindo na mwanasosholaiti Fahyvanny kwa mara nyingine tena amekuwa kioja cha kuzungumizwa mitandaoni baada ya kudai kwamba uzuri wake umeongezeka mara dufu na hivyo mahari imeongezeka kwa mwanqaume yeyote aliyekuwa na mipango ya kumchumbia.

Fahyvanny ambaye wengi walimjua kutokana na kuchumbiana na msanii Rayvanny na mpaka kurubuni jina la msanii huyo na kuunda lake kutokana nalo alisema kwamab uzuri wake kwa siku za hivi karibuni umezidi kunoga na bei ya mahari haitabaki pale ilipokuwa jana kwani nayo lazima itii na kuongezeka vile vile.

“Nyie nyie, naomba mahari iongezeke, sio kwa uzuri huu,” alisema kwa mikogo ya tausi.

Mashabiki wanaomfuatilia kwenye mtandao wa Instagram walionekana kumjibu makali mubashara huku wengi wakionekana kumsema kwamba hamna uzuri wowote bali ni vipodoshi tu ndio vimechangia kwa asilimia kubwa ya uzuri wake.

“Mahari gani wakati hapo ukinyeshewa na mvua make up inavuja na unakuwa mwingine kioja, hapo bado sijaja kwenye filter za simu au basi tu,” mmoja alimsimanga.

Fahyvanny walikuwa na mahusiano ya muda mrefu na msanii Rayvanny mpaka mwaka wa 2019 ambapo alitangaza kuachana na msanii huyo baada ya kubarikiwa na mtoto mmoja.

Za chini ya zulia zilidai kwamba kuvunjika kwa mahusiano yao kulitokana na mwanadada aliyekuwa akicheza kweney video ya ‘I Love You’ ya msanii huyo ila mwaandada huyo alikuja akaweka bayana kwamba hakuwa anachumbiana na Rayvanny. Aidha, msanii huyo hajawahi kujitokeza hadharani kupinga wala kukiri madai hayo.

Fahyvanny anajiongezea mahari wakati ambapo nchini kenya, mwenzake Pritty Vishy ambaye alikuwa mchumba wa msanii Stivo Simle Boy siku za hivi karibuni pia amegonga vichwa vya habari baada ya kudai kwamba kwa uzuri alio nao mahari yake inasimamia shilingi milioni mbili pesa za Kenya.

Vishy ambaye miezi mitatu iliyopita waliachana na Simple Boy kwa kuchafuliana majina mitandaoni alisema mwanaume yeyote asijaribu kupeleka posa kama hana uhakika wa milioni mbili za mahari.

Wikendi iliyopita walionekana na mwanamuziki Madini Classic aliyedai kwamba yuko tayari kulipa mahari ya milioni 4 ili kumchukua Vishy kama mkewe, video fulani ilisambazwa ikidai wawili hao tayari washafika kwa wazazi na mahari kulipwa kama si kuzungumziwa kwa kina.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved