"Huyo bibi kizee hawezi kuzalia" Mr Pimbi amchamba Harmonize kuhusu Kajala

Alisema Harmonize hawezi mfikia Rayvanny kwa utajiri hata atuame vipi.

Muhtasari

• “Kwake inakuwa ni ngumu sana kukua kimuziki, muziki wake umeporomoka sasa hivi amebaki anategemea mwanamke" - Mr Pimbi

Muigizaji na mchekeshaji Mr Pimbi
Muigizaji na mchekeshaji Mr Pimbi
Image: Instagram///mrpimbi

Muigizaji mbilikimo kutoka Tanzania kwa jina Mr Pimbi amemvaa msanii Harmonize mubashara kwa kuondoka Wasafi kwa kashfa kubwa na kusema kwamba bosi huyo wa Konde Music Worldwide hawezi kamwe kumfikia kimuziki msanii Rayvanny ambaye ameondoka Wasafi wiki jana.

Akizungumza na waandishi wa habari za umbea, Mr Pimbi alisema kwamba Rayvanny ndiye msanii wa kipekee kutoka Afrika ambaye ametuzwa tuzo ya heshima kubwa ya BET na kusema kwamab licha ya mafanikio yake yote bado kijana katulia huku Harmonize bila tuzo yoyote ya maana nje ya Tanzania anatamba na kutanua kifua kweli huku akimkashfu Diamond.

Mr Pimbi alisema hata muziki wa Harmonize kwa sasa umeporomoka pakubwa na amebaki tu kumtegemea mwakamke Kajala ambaye kulingana na muigizaji huyo ni kama ajuza tu ambaye hawezi kumzalia Harmonize.

“Kwake inakuwa ni ngumu sana kukua kimuziki, muziki wake umeporomoka sasa hivi amebaki anategemea mwanamke. Sasa basi si unafaa unategemea mwanamke kabichi hivi, sasa unategemea ajuza, bibi kizee. Yule hata kumzalia hawezi, kwani ni uwongo, sayansi si ndio inasema hivo,” Mr Pimbi alifoka.

Muigizaji huyo mcheshi pia alizidi kumshambulia Harmonize huku akimpaisha Rayvanny kwa usanjari huo na kusema kwamba Vanny Boy amefanya mambo makubwa sana na msanii Macvoice ambaye alimleta kwenye gemu tayari ana mradi mkubwa sana wa ngoma na msanii kutoka Marekani, Justine Bieber.

Alisema kwamba msanii Rayvanny ni Tajiri mkubwa kupindukia sema tu ni vile hapendi kelele na miyeyusho ya mitandaoni kujionesha