(Video) "Kondomu hapana! Hata Mungu amekataa kutumia" = Stevo Simple Boy

Msanii huyo aliwahi kiri kwamba yeye ni bikra.

Muhtasari

• Kulingana na Stevo, hakuna haja ya matumizi ya mipira ya kinga kwani watu wanafaa kuaminiana.

Mwanamuziki gumzo pevu humu nchini Stevo Simple Boy kwa mara nyingine tena amezua mjadala kweney mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba hawezi kamwe kutumia mipira ya kinga wakati wat endo la ndoa akidai kwamba hata Mungu mwenyewe amekataa binadamu kutumia kondomu wakati wa kushiriki kitendo cha mapenzi.

Katika video moja ambayo imepakiwa mitandaoni, mwanadada mmoja anaonekana akimuuliza wazo lake kuhusu matumizi ya kondomu na Simple Boy kwa haraka anadakia kwa kukataa kabisa.

“Stevo uko kwenye upande wa kukubali matumizi ya kondomu?” anauliza mwanadada huyo.

“Hapan! Kondomu Hapana. Hata Mwenyezi Mungu amesema tusitumie kondomu. Haijaandikwa kwa Biblia lakini hatufai kutumia,” Stevo Simple Boy alikomalia jibu lake.

Akiulizwa atoe sababu zake kupinga matumizi ya mipira ya kinga, mwanamuziki huyo alisema kwamba hakuna haja kwani watu wanafaa kutafuta watu ambao wanaaminiana na kupendana basi.

“Kama umepata yule mwenye anakupenda, na wewe umpende basi! Hakuna haja ya kondomu,” msanii huyo wa ‘Mihadarati’ akisisitiza msimamo wake.

Ikumbukwe siku kadhaa nyuma baada ya kutengana na mwanamitindo Pritty Vishy, mwanadada huyo alifichua kwamba katika muda wote walikuwa kwenye mahusiano, hawakuwahi kushiriki tendo la ndoa hata mara moja akisema kwamba mwanamuziki huyo alikuwa mwoga na hakuwahi mkaribia.

Kwa upande wake Stevo alidhibitisha madai hayo na kukiri kwamba yeye ni bikra, kwa maaan kwamab hajawahi onana kimwili na mwanamke yeyote tangu kuzaliwa kwake na hivyo kumtuhumu Vishy kwa kuchepuka nje ya mahusiano yao na wanaume zaidi ya hamsini.

Mtunzi huyo wa kibao ‘Freshi Barida’ alituhumiwa na Vishy kwamba alichepuka na mwanamuziki wa kike kutoka pwani kwa jina Adasa na kusema ndicho chanzo kikubwa cha kutengana naye, ila Stevo alipinga madai hayo na kusema kwamba ni mradi wa collabo tu uliompeleka Pwani ambapo alirudi na maneno hayo ya ‘Freshi Barida’ yaliyoshabikiwa na wengi nchini mpaka kupelekea yeye kufanya ngoma kwa jina hiyo.

Baadae pia baada ya ngoma ya awali kufanya vizuri, alishirikiana na wasanii wenzake kufanya remix ya kibao hicho wiki jana ambacyo pia inazidi kukwea kwenye chati za muziki humu nchini kwa kasi ya duma.

Msanii huyo pia alisisitiza msimamo wake kwamba hajui mtindo wowote wa kushiriki ngono kwani yeye bado ni bikra. Ila aliwahi sema kwamab ukifika muda maalum wa kuwa na familia basi angependa sana kuwa na watoto wengi, zaidi ya hamsini kwa idadi ya kukadria.