logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(Video) DJ Shiti aeleza alivyotuma ujumbe wa mapenzi kimakosa kwa rafiki wa babake

Ilikuwa sikukuu ya Valentino ambapo Shiti alichukua simu ya babake kumtumia mpenzi wake ujumbe, kwa bahati mbaya ujumbe ukaenda kwa rafiki wa kiume wa babake.

image
na Davis Ojiambo

Burudani21 July 2022 - 08:51

Muhtasari


  • • Rafiki wa babake akapata ujumbe na kushangaa ujumbe ule ambapo alipiga simu ndio akaelezewa ujumbe ulitumwa na kijana.

Mchekeshaji maarufu nchini Kenya, DJ Shiti ameelezea jinsi ambavyo wakati mmoja alijikuta pabaya baada ya kutumia simu ya babake kutuma ujumbe wa kimapenzi kwa rafiki wa babake.

Shiti alisema kwamab hali hiyo ilimtokea wakati ambapo hakuwa na simu na hali ilikuwa mbaya na ngumu kupata moja ndio akaamua kutumia ya babake kuzungumza na mpenzi wake, kwqa sababu siku hiyo ilikuwa siku kuu ya wapendanao duniani, Valentines Day.

“Ilikuwa ni sikukuu ya Valentino, watu waantumia wapenzi wao jumbe nzuri za kuwasherehekea na kuwatakia kila la kheri siku hiyo ya mapenzi, na mimi nakachukua simu ya babangu kumtumia mpenzi wangu ujumbe. Kumbe ule ujumbe haukuendea mpenzi wangu bana, uliendea rafiki wa babangu,” DJ Shiti alielezea.

Mchekeshaji huyo alielezea kwamab rafiki huyo wa babake alikuwa wa jinsia ya kiume na kuona ule ujumbe wa kimapenzi pengine alifikiria babake DJ Shiti amegeuka kuwa shoga na hapo akapiga simu kutaka kujua kiini na lengo la ujumbe ule wa kimapenzi.

“Yule rafikiye babangu akampigia simu baba, Hello bwana Richard, huu ni ujumbe gani unaniandikia? Baba akuliza, ni ile yetu ya wazee, yule rafiki yake akamuambia Hapana, umeniandikia kwamba ungetamani kunishikilia kwqa nguvu usiku wa leo,” DJ Shiti alisema baina ya utani.

Hapo ndio babake Shiti alipandwa na mori kama Mmasai na kusema kwa hasira kwamba ni kijana yake ambaye ni Shiti aliyechukua simu yake ili kuandikia mpenzi wake ujumbe.

Shiti alimsifia babake kwa utu uzima aliouonesha kwani hakumpayukia kwa sababu alikuwa amejua kijana wake ashakomaa na kuwa na mpenzi halikuwa jambo geni.

Kisa kipi kimewahi kutokea ukituma ukajipata umetuma ujumbe kwa mtu tofauti?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved