"Kifuniko cha asali" Babu Owino afurahia kuinua chupi

Babu Owino alikuwa mbunge kwa mara ya kwanza mwaka 2017 akiwakilisha eneo la Embakasi East.

Muhtasari

• Mbunge huyo anatarajia ushindani mkali kutoka kwa Francis Mureithi wa UDA ambaye mpaka sasa kura za maoni zinamuweka mbele ya Owino.

Mbunge wa Embakasi East Babu Owino akionesha mwanandani ya kike.
Mbunge wa Embakasi East Babu Owino akionesha mwanandani ya kike.
Image: Facebook//Babu Owino

Mwanasiasa kijana ambaye pia ni mbunge wa Embakasi ya Mashariki Babu Owino kwa mara nyingine tena amedhihirisha wazi vituko vyake kwenye mtandao wa Facebook baada ya kupakia picha ya nguo ya mwanandani ya kike.

Babu Owino ambaye kwenye picha hiyo anaonekana akiinua juu nguo hiyo ya ndani ya wanawake huku akiwa amejawa na tabasamu ghaya, Babu anaonekana kuwa katika moja ya msururu wa kampeni zake akilenga kutetea nyadhifa ya ubunge eneo hilo linalokumbwa na ushindani mkali kutoka chaguzi za zwali.

“Kifuniko cha asali,” Babu Owino aliambatanisha maelezo haya kwenye picha hizo.

Maneno haya ya Owino akifuatisha na picha hiyo ya mwanandani ya kike yalizua maoni kinzani kutoka kwa wafuasi wake ambao wengine walizua utani huku wengine wakimzomea kwamba hana maadili mema ya kuwa kiongozi.

“Sikutarajia hili kutoka kwa kiongozi kama wewe Babu unachoma,” mmoja kwa jina la Abraham Lelei Jr aliandika.

“Acheni za hovyo, hapa ndio gumzo huanzia. Kama mnaona haya kwa Babu kuinua nguo kama hiyo mchana peupe basi ina maana hamko tayari kabisa kulea kizazi cha sasa. Ni nguo tu kama nguo zingine,” mmoja kwa jina Waniru Kuria alimtetea Owino.

Mwanasiasa huyo ambaye ni mtetezi mkali wa sera za kinara wa ODM Raila Odinga aliingia katika siasa mwaka wa 2017 na kuwania ubunge wa Embakasi ya Mashariki kwa tikiti ya chama cha ODM ambapo alimshinda kwa kura chache mshindani wake wa karibu kipindi hicho akiwa Jubilee, Francis Mureithi.

Owino alaenga kutetea kiti hicho kwa mara ya pili mtawalia tena kupitia tikiti ya ODM huku mpinzani wake Mureithi wa UDA akimkimbiza kwa ukaribu mno kulingana na kura za maoni.

Babu Owino aliwahi kuhudumu kwa muda mrefu kama kiongozi wa muungano wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kujitosa kwenye siasa za nchi mwaka 2017