Kumekucha! Sauti ya Nandy akitoa maagizo ya Zuchu kuchafuliwa jina yavujishwa

Kwenye sauti hiyo, Nandy anasikika akimpa Mwijaku maagizo jinsi ya kuandika ujumbe wa kumkandia chini Zuchu.

Muhtasari

• Maagizo hayo ni kutokana na Zuchu kuchukua dili la kuwa balozi wa kampuni ya vileo, dili ambalo Zuchu alidaiwa kulikataa kwa misingi ya kidini.

Wasanii malkia wa bongo fleva Zuchu na Nandy
Wasanii malkia wa bongo fleva Zuchu na Nandy
Image: Instagram

Siku fulani nyuma msanii Zuchu aliwahi weka wazi kwamab alifuatwa na kampuni fulani ya kuuza vileo ili kumpa dili ya kuwa balozi wa matangazo yao ya kibiashara ila akakataa kutokana na kwamba dini yake ya Kiislamu haioni kuwa sahihi mambo kama hayo ya kutangaza bidhaa zisizompendeza Mungu.

Sasa jipya kabisa limeibuka baada ya sauti inayodaiwa kuwa ya msanii Nandy akisikika akimueleza mtangazaji mmbea Mwijaku kumkandia chini Zuchu na kumchafua kwamba si eti alikataa dili lile bali dili lenyewe hakuitwa wala kulipata.

Sauti hiyo inayosemekana kuwa ya Nandy inazidi kutoa maelezo kwa Mwijaku na kumtaka asambaze uvumi kwamba Zuchu hakuitiwa mahojiano ya dili hiyo ya ubalozi wa kampuni ya vileo bali nandy alipewa moja kwa moja baada ya kukosekana mshindani kwenye Mahojiano ya kupata balozi wa matangazo ya biashara ya kampuni hiyo.

“Halafu Mwijaku, kwenye kwamba walikuwa walikuwemo wasanii wangapi akiwemo Zuchu, andika hivi, hiyo hoja kwanza itoe na uandike hakuna mtu ambaye atapewa dili la hela nyingi, alikataa yeye, haswa suala la pombe. Isionekane hivo kwa sababu mtu atajua kwamba tumesema zaidi yaani tumefichua mbala maelezo ya ndani,” sauti hiyo inayoaminika kuwa ya Nandy inasikika akitoa maelezo ya jinsi ujumbe wa kumchorea nje Zuchu utakavyotungwa kwa maslahi yake mwenyewe.

Vita baridi vya wasanii hao wawili wa kike wanaopambana sana kuonekana kwenye ramani ya muziki wa Afrika Mashariki inakuja wakati ambapo bado wafuasi na wapenzi wa miziki ya Afrika mashariki wako katika mijadala mikali ya kutambua ni nani malkia wa muziki kati ya Zuchu na Nandy.

Wikendi hii msanii Nandy anatarajiwa kufanya tamasha lake la kila mwaka almaarufu nandy Festival huko Songea, baada ya kutofanyika kwa miaka miwili iliyopita kutokana na ujio wa janga la Corona.

Wasanii malkia wa bongo fleva Zuchu na Nandy
Wasanii malkia wa bongo fleva Zuchu na Nandy
Image: Instagram
Wasanii malkia wa bongo fleva Zuchu na Nandy
Wasanii malkia wa bongo fleva Zuchu na Nandy
Image: Instagram