Mcheza santuri wa Mugithi, DJ Fatxo kwa mara nyingine tena mwaka huu ameudhihirishia ulimwengu kwamba ni mwaka wake wa kufanya mambo makubwa maishani mwake baada ya kununua gari jipya.
Akionesha furaha yake kupitia Instagram, Fatxo amesema uzinduzi wa gari lake jipya ni baraka tele kutoka kwa Mungu na pia amewashukuru mashabiki wake wote ambao wamekuwa wakimpa shavu la sapoti.
“Nimezindua gari langu jipya na namshukuru Mungu kwa upendo na baraka zake zisizo na masharti. Naiweka wakfu Gari hili kwa Mungu, mashabiki wangu wasio na shaka ambao wameendelea kuunga mkono sanaa na muziki wangu na hatimaye kwa yeyote anayepitia mapambano na ndoto yake,” DJ Fatxo aliandika huku akifuatisha rundo la picha akiwa kwenye gari hilo jipya kabisa.
Alichukua fursa hiyo kuwashukuru wote na pia kutoa himitizo kwa mashabiki zake ambao aliwaambia mtu yeyote mwenye ndoto basi asiwahi kufa moyo kwani ipo siku mambo yatatengemaa. Alifichua kwamab gari hilo lina nambari za usajiri mpya kabisa za KDJ.
“Nataka kumtia moyo mtu yeyote ambaye ana ndoto kamwe asipoteze matumaini katika itikadi ya kuwa mshindi!! Hatimaye, kumbuka daima"Maisha yaliyo mbele yako ni muhimu zaidi kuliko maisha nyuma yako"! M.r Dj anafuraha kuwa na KDJ,” Fatxo aliandika.
Ikumbukwe miezi kadhaa iliyopita mcheza santuri huyo aliwakabidhi wazazi wake nyumba ya kifahari aliyowajengea na kuwawekea vitu vya ndani ambapo siku ya kusherehekea wapendanao duniani, Valentiono, aliwasherehekea wazazi kwa kuwakabidhi zawadi hiyo ya kudumu.
Wiki chache baadae tena alimshangaza mpenzi wake kwa kumnunulia gari wakati anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.