Je, kwa nini Diamond siku hizi hapati 'views' nyingi YouTube? Mashabiki wamemchoka?

Juzi Diamond aliachia video mbili kutoka kwa albamu yake nusu ya FOA na mpaka sasa hazijafanya vizuri YouTube.

Muhtasari

• Watu wametoa maoni baada ya video za 'Somebody' na 'Melody' kutofanya vizuri kwa siku za kwanza mbili tangu kuziachia juzi.

Msanii Diamond Platnumz kwenye ziara ya kimuziki bara Uropa
Msanii Diamond Platnumz kwenye ziara ya kimuziki bara Uropa
Image: Instagram//DiamondPlatnumz

Alhamis msanii anayejiita mfalme wa Bongo Fleva Diamond Platnumz aliachia video za ngoma mbii kutoka kwa albamu yake fupi ya FOA. Kama kawaida kawaida, wengi walitegemea video hizo zingekimbia na kupaa kwenye kupata idadi ya watazamaji kwa wepesi mno lakini sasa hilo limeonekana kuwa kinaya.

Zaidi ya saa 24 tangu kuachia video hizo za ‘Somebody’ na ‘Melody’ ngoma hizo hazijafanya vizuri hata kidogo na mpaka Ijumaa jioni ngoma ya ‘somebody’ ilikuwa imejizolea views 498K pekee, kinyme na matarajio ya wengi waliotegemea ngoma hiyo kupiga zaidi ya views milioni 2 kuendelea kama ambavyo ngoma nyingine kutoka kwa msanii huyo zimekuwa zikifanya.

Ngoma ya ‘Melody ambayo ni collabo na msanii Jaywillz nayo haijaenda mbali vile kwani imekwama kwa views 452K.

Kudorora kwa utazamaji na ufuatiliaji wa kazi za Diamond katika siku za hivi karibuni kumezua mjadaal mkali mitandqaoni huku baadhi wakihisi huenda watu wamechoka na msanii huyo au pengine zile mbinu alizokuwa akitumia kughushi takwimu za watazamaji YouTube amezikoma.

Wengine walihisi video hizo zimefanya vibaya kutokana na kwamab hakukuwa na kiki na zilitoka kimya kimya ndio maana pengine watu wengi hawajajua na kuzitafuta huku wengine wakisema msanii Harmonize anakuja kwa kasi na kumuacha nyuma.

“Tumezoea kuona Diamond akipata views nyingi sana kuliko msanii yoyote yule Kusini mwa Jangwa la Sahara lakini hivi sasa mambo yamekuwa tofauti mno. Ni kama Harmonize anakuja kwa speed kali mno, tunaona video zake hivi karibuni zikipata Views nyingi mno kuliko hizi za Diamond Platnumz. Je tatizo ni nini?, watu wamemchoka Diamond? au kwasababu video hizi zimetoka bila kiki kwanza, ndio maana hazijapata watazamaji wengi?,” mdau mmoja aliuliza.

Mwingine alizua utani hapo na kuwaambia mashabiki wa msanii huyo kuacha masihara na kuingia YouTube ili kumpaisha mfalme wao na kumtoa katika mavumbi ya aibu.

“Haya mashabiki wa dabiliu sibii achene umbea nendeni mkaangalie wimbo wa bosi wenu maana yameshaa pita masaa zaidi ya 10 lakini views ni laki mbili tu,” mdau kwa jina DJ Amani the mix masters Tz alitania.

"Siku hizi hatoi mziki mzuri kama zamani.. Zamani akikua anaimba sana tena sanaaa.. Sasa hivi Tembo anaimba babda Na Vany nae anakuja kivingine.. Dai atulie tu kimziki aangalie wanae yy ale pesa zake akizoekeza.. Mzik tena basi.." mwingine alidakia.