"Nafunga ndoa na wewe hivi karibuni na sitoku'cheat" Harmonize amwambia Kajala

Mwezi mmoja uliopita, Harmonize alimvisha Kajala pete ya uchumba.

Muhtasari

• "Kukuoa ni ndoto na nashukuru Mungu tunakaribia hapo." - Harmonize

Msanii Harmonize akimsherehekea mchumba wake Fridah Kajala Masanja
Msanii Harmonize akimsherehekea mchumba wake Fridah Kajala Masanja
Image: iNSTAGRAM//HARMONIZE

Msanii wa kizazi kipya ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music World Wide, Harmonize amemsherehekea mpenzi wake Frida Kajala kwa ujumbe maalum siku yake ya kuzaliwa.

Kupitia Instagram yake, Harmonize alimsherehekea muigizaji mkongwe mchumba wake Kajala Masanja kwa kumwambia kwamba atagemea kumuoa hivi karibuni na hata kumuahidi kwamba katu hatochepuka kabisa kwani makosa kama hayo yalimfanya kidogo amkose kabisa mwaka jana.

Harmonize kweney ujumbe huo mrefu alimwambia kwamab kumfanya meneja wa kazi zake za kimuziki ni ishara tosha kuonesha kiasi gani anamkubali, kumuamini na kumpenda bila kujali maneno ya watu kuhusu tofauti kati ya umri wao.

“Kheri njema ya siku yako ya kuzaliwa mpenzi wa maisha yangu MISS BANTU. Kukuoa ni ndoto na nashukuru Mungu tunakaribia hapo. Kukufanya meneja wa kazi zangu za kimuziki inaonesha kiasi gani nakuamini na kiasi gani wewe ni wa muhimu katika maisha yangu. Najua wengi wanakubeza, wengi hawaamini kwamba unaweza simama imara. Katika kazi hii yenye ugumu wake, ndio wewe unaweza,” Harmonize alitiririkwa mishororo ya mahaba.

Harmonize alifungukia kwamba alimfanya akang’aa tena kama dhahabu wakati maisha yake yalikuwa yanaona kiza kinene mbele na pia kusema kwamba Kajala alimfanya kuwaheshimu watu wa jinsia ya kike kwa kiasi kikubwa mno.

“Ulinifanya nikang’ara tena, nakupenda na kuwaheshimu wanawake wengine ndicho kitu nimechagua. Ndio muziki ni kazi yangu na mashabiki wa kike ndio nguzo yangu ila sidhani kila mwanamke anayenishabikia basi ananitaka kimapenzi. Nimegundua kundi la mashabiki zangu wengi ni watu wanaojitambua na wanajua tofauti ya maisha, ushabiki na anasa,” Harmonize alizidi kusema.

Msanii huyo pia alikula Yamini kwamba aliwahi jisemea kwamba siku atapata mpenzi wa kikweli basi atatulia kabisa na yeye tayari kwa kajala keshanasa kung’atuka ni mwiko.

“Nilijiwekea Siku Nitakapo Pata Chaguo La Moyo Wangu Mtuu Aliejitoa Kupambana Vita Vyangu Sitojali Ni wapi Sangapi Nafanya Kazi Gani Muuni Nitampatia MOYO natulia Zangu na mwisho wa siku ndio hii hapa. Nakupenda sana mwanakwetu na acha tufanye maisha pamoja kajala,” alimaliza Harmonize.

Hrmonize mwezi mmoja uliopita alimvisha pete ya uchumba Kajala katika tafrija la kipekee lililosimamisha mitandao ya kijamii.