(Video) "Watoto wangu walilia nilipowaambia niko mjamzito" - Diana Marua

Wiki jana Diana na Bahati walitangaza kwamab wanatarajia mtoto wao wa tatu.

Muhtasari

• Pia alisema wanafnyakazi wake wa ndani pamoja na dadake walishindwa kuzuia machozi yao walipofahamishwa habari za ujauzito.

Mkuza mudhui wa YouTube na mwanamuziki wa kuchana mistari, Diana Marua bado anazidi kutamba kuhusu ujuauzito wake, wiki moja baada ya kuweka wazi kwamba yeye na mumewe Bahati wanatarajia mtoto wa tatu.

Katika video ambayo aliipakia kwenye YouTube yake, Diana Marua alisema kwamba alipowambia watu wake wa karibu kwamba alikuwa mjamzito, walishtuka mpaka wengine kutokwa na machozi ya furaha.

Diana Marua alisema kwamba hata watoto wake walipojua kwamba ana ujauzito wa mnuna wao, walitokwa na machozi ya kutoamini, mpaka akapakia video ya kuonesha jinsi walivyopatwa na mshtuko wa habari hizo.

“Weeeeeeeuuuuuhhhh, machozi yalikuwa mengi sana kwenye video ya Leo ya Kipindi changu cha Mimba, Sehemu ya 4. Mwanangu @Morgan_bahati alishindwa kuyazuia machozi yake alipojua kuwa Mama ana mtoto nambari 3 njiani,” Diana Marua aliandika kwenye video hiyo ya Instagram.

Pia alisema machozi hayo yaliwatoka dada yake pamoja na wafanyikazi wake wa ndani ambao hawakuamini kwamba kwa mara nyingine mtoto anatarajia.

“Niliamua kuwaambia wafanyikazi wangu wa kazi za ndani, dada yangu @glamby_varl na watoto wangu kuhusu baraka mpya na kusema maoni yao yanakosa bei ya kutajiwa ni maneno ya chini!” Diana B alisema.

Diana B ni mmoja wa waundaji wakuu wa maudhui na udhihirisho wa ujauzito ulisababisha familia yake kujumuika naye. Alirekodi maoni ya wanafamilia yake wakati wa mshangao; na watoto wake walikuwa wakibubujikwa na machozi walipojifunza kuhusu hilo zaidi ya wote, Morgan Bahati.

Marua na mumewe Bahati walitangaza wiki moja iliyopita habari hizo mpya ambapo siku chache baadae waliachia kibao kwa jina Nakulombotov.