logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Pengine mimi si mtu mzuri kwako lakini utanikumbuka" Jimal amwandikia Amira

“Pengine mimi si mtu mzuri katika maisha yako. Lakini siku moja utasikia jina langu likitajwa na utasema, kweli amekuwa tofauti, alibadilika,” Maneno hayo kwenye instastory ya Jimal

image
na Radio Jambo

Yanayojiri24 July 2022 - 00:59

Muhtasari


• Katika siku za hivi karibuni, Jimal ameonekana kuwa mweney mawazo baada ya kuachana na wapenzi wake wote.

Mfanyabiashara Jimal Rohosafi akionekana mwenye mawazo tumbi nzima

Mfanyabiashara na msimamizi wa magari ya uchukuzi wa umma jijini Nairobi, Jimal Rohosafi anazidi kulia upweke wiki moja baada ya msamaha wake kwa aliyekuwa mke wake wa kwanza, Amira kufuma kwenye jabali kavu.

Wiki jana, Jimal aliamua kuweka kando ushababi wa kiume na kujuta kwa kile alichomfanyia mke wake wa ndoa kwa kutoka kimapenzi na mwanamitindo Amber Ray ambapo alimdhalilisha mkewe bayana.

Jimal alimuomba mkewe msamaha na kumwahidi kwamab amebadilika na angependa kupewa nafasi ya pili kudhuhirisha mabadiliko yake kwa mkewe kama watarudiana na kuijenga familia pamoja.

Naomba radhi kwa kukukosea heshima, kukuaibisha, kwa kukuumiza, kwa maumivu yote na kwa huzuni niliyokuletea. Samahani kwa nyakati zote ambazo sijawa mwanaume niliyeahidi kuwa," Jimal alimuandikia mkewe.

Mkewe siku moja baadae alionekana kujibu msamaha huo kwa kusema kwamba alidhalilika sana kwa vitendo vya Jimal kutoka wazi kimapenzi na michepuko na mpaka kuwakubalia wanawake hao kumdhalilisha wazi wazi bila yeye kumtetea. Alionekana kuukataa msamaha ule kwa usemi kwamab vidonda vingine ni vya kuishi navyo wala haviwezi pona.

Sasa Jimal bado anazidi kujitia shime na matumaini kwamba huenda siku moja msamaha wake utakubalika ambapo amepakia picha yenye maneno ya kujuta kwenye instastory yake akisema kwamba anahitaji kupewa nafasi kudhihirisha kwamba kweli amebadilika.

“Pengine mimi si mtu mzuri katika maisha yako. Lakini siku moja utasikia jina langu likitajwa na utasema, kweli amekuwa tofauti, alibadilika,” Maneno hayo kwenye instastory ya Jimal yalisoma.

Kama msemo wa mpanda farasi wawili hupasuka msamba yangekuwa hufananishwa na mtu basi bila shaka angekuwa Jimal, kwani mwaka jana alijaribu kuwa na mahusiano na mkewe pamoja na mwanamitindo Amber Ray kwa waakti mmoja lakini inasikitisha kwamba mahusiano yote yalimtoka puani na wote walimuacha, sasa analia, sasa anajuta na kutaka kurudi kwa mke wake wa halali ambaye walikuwa wamefanikiwa watoto wawili na yeye.

Mapema mwaka huu Amber Ray alitangaza kushiba mahusiano na Jimal na mpaka akapakia video kwenye Instagram yake akiifuta tattoo ya mfanyabiashara huyo Tajiri aliyoichora kwenye mgongo wake kama njia moja ya kudhihirisha mapenzi yake kwake baada ya kumnyakua kutoka kwa mke wake wa kwanza Amira.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved