(Video) "Unafanya uzazi kuwa rahisi" Akothee amsherehekea bintiye kwa kujinunulia gari

Vasha Okello alijinunulia gari kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa.

Muhtasari

• Vasha Okello ambaye pia ni mkurugenzi katika kampuni ya mamake ya Akothee Safaris alisherehekea siku yake ya kuzaliwa wiki sita zilizopita.

• Jana, amepakia video kweney instagram akisema amejinunulia gari kama zawadi ya kufikisha miaka 25.

Vesha Okello ambaye nmwanawe mfanyibiashara na mwanamuziki Akothee amejinunua gari jipya kama zawadi ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vesha ambaye pia ndiye mkurugenzi mkuu katika kampuni inayomilikiwa na mamake ya kitalii, Akothe Safaris alifurahia na kujisherehekea mwenyewe kwa kujinunulia zawadi hiyo kubwa kabla ya mtu yeyote kumzawidi.

“Hatimaye nilijizawadi mwenyewe mtoto huyu kama zawadi ya siku yangu ya kuzaliwa,” aliandika kwenye video hiyo inayomuonesha akiwa kweney hilo gari lililokuwa limepambwa maua si haba.

Watu wa kwanza kumsherehekea na kumpa hongera kwa zawadi hiyo walikuwa ni familia yake ambapo mamake na dadake mkubwa, Rue Baby walimpongeza na kumtakia kila la kheri huku wakimwambia anastahili zawadi zaidi ya hiyo kwa ile kazi ambayo amefanya kustawisha kampuni hiyo ya mamake.

“Eeeee, hata sijasikia vibaya, niruhusu nikupigie makofi mpenzi wangu, unafanya uzazi uonekane rahisi, nakupenda waa hata sisi familia unatunyima memo?” Akothee alimwandikia huku akimtania.

“Hongera mdogo wangu, unastahili hili,” dadake Rue Baby aliandika.

Akothee ambaye amebarikiwa na watoto watano kwa sasa yupo nchini Ufaransa akiandamana na mwanawe Rue Baby ambapo alisema ako ziarani barani Ulaya kwa ajili ya kutafuta mimba ya mtoto wake wa sita, mimba ambayo alidokeza kwamba atawekewa mbegu za kiume na wala si kushiriki tendo la ndoa.

Mwanamama huyo ambaye juzi alisherehekea miaka 41 aliwahi dokeza kwamba kabla afike miaka 45 ambayo alisema ndio umri wake rasmi wa kustaafu kutoka muziki na umaarufu wa mitandaoni, alisema atapata mtoto mmoja wa mwisho ambaye sasa yupo mbioni kumtafuta ulaya.

Kwa sasa, Akothee tayari ameshaachia kitabu kinachozungumzia maisha yake kijumla na amedokeza kwamab mwaka kesho mwezi Februari atafungua shule yake mpya ambayo itakuwa inatoa mafunzo kwa watoto kutoka familia zisizojiweza, katika kile alisema ni kuwezesha kila mtu kupata ‘angalau elimu ya kujua kuandika na kusoma’

Wiki jana Akothee alidokeza mitandaoni kuhusu ugomvi unaendelea katika familia na ndugu zake ambapo alisema kunqa baadhi ya wanafamilia wake wanamuonea gere kwa mafanikio yake makubwa maishani licha ya kuwa mama wa kujitegemea bila mume, na watoto watano juu.