"Hii picha ilipigwa siku ya giza zaidi kwetu. Saa 2 baada ya kumlaza mama yetu" - Nana Owiti

Nana Owiti aliwashangaza wengi baada ya kupakia picha ya TBT akisema ni saa chache tu baada ya kumzika mama yao miaka 15 iliyopita.

Muhtasari

• "Siku nyingi, miezi na hata miaka iliyofuata ilikuwa ngumu zaidi" Owiti alikumbuka.

Mtangazaji wa runinga na dadake mdogo Portia Hagusu katika picha ya zamani wakimzika mama yao
Mtangazaji wa runinga na dadake mdogo Portia Hagusu katika picha ya zamani wakimzika mama yao
Image: Instagram//NanaOwiti

Mtanagzaji wa runinga ambaye ni mke wa mwanamuziki King Kaka, Nana Owiti amewaacha wanamitandao katika hali ya kustaajabu mambo makubwa ambayo Mungu anaweza mfanyia mja wake, baada ya kupakia picha za utotoni akiwa na dadake Portia Hagusu.

Kweney picha hizo amabzo ameziakia kulinganisha kitambo hicho na sasa hivi, Nana owiti amefichua kwamba picha hiyo ya zamani ni moja ya picha inayomkumbusha tukio la kiza kinene sana katika maisha ya familia yao kwani ilichukuliwa saa chache tu kabla ya kumzika mama yao mzazi.

“Amini usiamini picha ya kwanza ilipigwa katika moja ya siku ya GIZA ZAIDI ya maisha yetu. Chini ya saa 2 baada ya kumlaza mama yetu. Athari zisizoweza kudhibitiwa za kifo na hasara. Tuangalie tukiwa tumesimama kwa hofu ya kupepesa macho tukitazama shimo tupu ambalo ni maisha yetu. Alfajiri ya ukweli mpya na kawaida mpya.. Mwili kuzizima kote” aliandika Owiti.

Mtangazaji huyo ambaye umaarufu wake uliongezeka katika kipindi cha udaku kwenye runinga moja humu nchini alizidi kuelezea matukio yaliyojiri baada ya kumpoteza mama yao na jinsi kila kitu kilionekana tofauti ghafla.

“Huko nilikuwa .. kijana aliyetupwa kwenye njia panda, sio tu kujiinua mwenyewe lakini kwa haraka kuingia kwenye viatu vya mama yangu kwa kumlea mtoto wa miaka 9 na kutunza nyumba. Tuangalie, Tumechanganyikiwa na bado tulitabasamu. Siku nyingi, miezi na hata miaka iliyofuata ilikuwa ngumu zaidi, ngumu sana lakini Mungu alitupata ingawa wakati wa huzuni kuna jaribu la imani na shaka ya uaminifu huja kubisha bila shaka,” Nana Owiti alikumbuka kwenye ujumbe huo wenye simanzi ndani yake.

Alikuwa akizungumza baada ya mumewe kutambulisha rasmi filamu yake ya Kam Tupe ambayo alisema ilitoka kuhitimiza miaka 15 tangu kifo cha mamake ambapo walijumuika wote kama familia ya pande zote mbili ili kusherehekea si tu kifo cha mama yao bali pia hatua kubwa ya King Kaka kuzindua filamu.

Nana Owiti alidokeza kwamab kipindi hicho cha majonzi kilimbadilisha kabisa mpaka kumpa kiwewe amabcho alidokeza kwamba hali hiyo humbadilisha mtu kabisa, na pia kusema kwamba hata katika kifo bado wanaamini kama familia wamemfanya mama yao kujivunia.

“Pia, kiwewe hutubadilisha kabisa. Huwezi kuwa wewe yule wa zamani. Kwa wale wote wanaoshinda kiwewe, Wewe ni MSHINDI. Sio rahisi, najua lakini bado tunaendelea mbele. Hata hivyo, tulifanya hivyo Mama. Najua tunakupa tabasamu la kujivunia,” Owiti alisema.