Msanii wa kike kutoka Tanzania, Chemical_tz atangaza kujioa mwenyewe

Wikendi iliyopita picha za msanii huyo akiwa kwenye shela la harusi zilisambaa mitandaoni.

Muhtasari

• Msanii huyo alisema kwamba watu wasikuwe wanadadisi sana ni kwa nini hawajamuona bwana harusi na kuweka wazi alijioa mwenyewe.

Msanii wa kuchana mistari, Chemical
Msanii wa kuchana mistari, Chemical
Image: iNSTAGRAM//cHEMICAL

Msanii wa kike nguli wa kuchana mistari kutoka nchini Tanzania, Chemical wikendi iliyopita palizuka picha yake akiwa amevalia joho la harusi kabisa ambapo wengi waling’aka kwamab hatimaye amepata mume na ametulia kwenye ndoa, kutakana na jinsi alivyojiremba kweney nguo ile ya harusi.

Sasa msanii huyo Jumanne katika mahojiano na kituo cha habari kimoja nchini Tanzania ameweka wazi kuhusu suala la ndoa na harusi ambapo mwanzo alianza kwa kudhibitisha kwamba kweli picha ile ni yake halisi wala haikufanyiwa uhariri wowote ili kumuonesha kwamba amevalia joho la harusi.

Ila swali ambalo lilikuwa linasumbua vichwa vya wambea wengi si tu nchini humo bali katika ukanda mzima wa Afrika mashariki ni kuhusu kutomuona bwana harusi ambaye hakuna hata picha moja Chemical alipakia wakiwa pamoja, ni ile tu yake yeye akiwa na maua na nguo ya harusi, jeupe pamoja na pete kuonekana kwenye kidole.

Msanii huyo katika mahojiano hayo aliwashangaza wengi alipodai kwamba kweli alifunga ndoa lakini hakufunga na mwanaume yeyote bali alijioa mwenyewe kwa kujiridhisha.

“Watu hawajamuona mume, wanauliza mume ni nani, nini. Ila mimi ile picha mnayoiona ndio hivyo, mimi nimejiona mwenyewe, nimeolewa na tasnia yangu ya muziki wangu,” alisikika akisema msanii huyo.

Huyu si msanii wa kwanza kutoka nchini humo kuibuka na madai ya vituko kwani wiki chache zilizopita itakumbukwa msanii Malkia Karen alikuja na jipya kabisa ambapo alipoulizwa baba wa mtoto wake wa kiume ambaye ako naye alisema ni mtoto aliyemzaa pasi na baba, yaani mtoto huyo alipatika bila kushiriki tendo la ndoa.

Msanii huyo alielezea zaidi kwamba alipata mtoto huyo kwa kuwekewa mbegu za kiume kwenye uke wake hospitalini kwa sababu alikuwa na uhitaji wa mtoto lakini hakufanikiwa kupata mwanaume wa kuzaa na yeye na ndio maana aliamua kuendea njia hiyo ya kufuru kupata mtoto kama yesu, pasi na kushiriki tendo.

Msanii Chemical aidha alisema kwamba picha hiyo inayozungushwa mitandaoni pia itatumika kama moja ya muonekano wa nje wa ngoma zake ambazo ameziachia jana, na watu kama wanataka kujua ukweli kama kweli kajioa mwenyewe basi wazisikilize ngoma na ukweli wote wataujua mule.