(Video) "Nahisi kupata mimba, hebu mnifanyie mambo" Sandra Dacha atania ujauzito wa Awiti

Awiti na Sandra Dacha ni marafiki wa muda mrefu na waliwahi fanya kazi ya uigizaji pamoja.

Muhtasari

• “Kati yangu na yeye ni nani mnaona atazaa wa kwanza?” Sandra Dacha aliuliza.

Muigizaji Sandra Dacha amepakia picha ya pamoja wakiwa na muigizaji mwenza, Awiti aliyejizolea umaarufu kutoka kwa maigizo ya The Real Househelps of Kawangware yaliyokuwa yakipeperushwa kwenye runinga moja ya humu nchini miaka michache iliyopita.

Katika picha hiyo, Awiti anaonekana akiwa na ujauzito mkubwa ambapo Dacha ametania mashabiki wake kuwauliza kati yake yeye na Awiti ni nani anaonekana kuzaa wa kwanza, kutokana na ukubwa wa mwili wake ambao haaibiki kujivunia licha ya watu kumburuza mitandaoni.

“Kati yangu na yeye ni nani mnaona atazaa wa kwanza?” Sandra Dacha aliuliza.

Waigizaji hao ambao waliwahi fanya kazi ya kuigiza pamoja ni marafiki wa muda mrefu na Awiti amekuwa akikosekana kweney mitandao ya kijamii ila sasa Dacha leo amefichua kwa kuonesha picha zake akiwa mjamzito.

Katika moja ya video ambazo pia muigizaji huyo mwenye umbo la bonge alipakia kwenye mitandao yake ya kijamii, alifanyqa utani kwa kusema kwamba jinsi Awiti anaonekana vizuri akiwa na mimba ile na yeye alihisi kutaka kuwa na mimba na kuwataka mashabiki wake kumfanyia mchakato wa kupata mimba.

“Aaaaah sasa nahisi kupata mimba haraka haraka! Ebu mnifanyie mamboz,” Sandra Dacha alitania huku wakimsherehekea Awiti kwa kulea mimba mpaka kiwango hicho cha kukaribia kutimiza miezi tisa.

Dacha alidhibitisha wiki chache zilizopita kwamba tayari ana mtoto wa miaka minane licha ya wengi kumuona kama hajawahi pitia mchakato wa kuzaa, ila aliwashangaza wengi alipopakia picha ya kijana huyo wake mkubwa akimtakia kila la kheri katika siku yake ya kuzaliwa.

Aidha, muigizaji huyo alisema kwamba yeye na mchekeshaji Akuku Danger hawawezi kuachana hata kwa dawa, licha ya kujua kwamba mcheshi huyo ana mke na mtoto ambaye alikuwa anapakia mpaka Dacha kwa wakati mmoja akalalamika akimtaka apunguze kumpakia mke wake kwani anajua kwamba yeye ni mpango wa kando lakini hawezi kumuacha.