Diamond amchora Zuchu kwenye T-sheti lake, aendeleza mjadala wa huba baina yao

Diamond na Zuchu wamekuwa wakioneshana mapenzi hadharani kwa vitendo licha ya kukataa kwa maneno.

Muhtasari

• Kuonekana kwa picha ya Zuchu kwenye nguo ya Diamond kulizua mjadala mkali mitandaoni baadhi wakisema ni kawaida huku wengine wakisema mapenzi yamekolea.

ZUCHU NA DIAMOND PLATNUMZ
Image: WASAFI/INSTAGRAM

Uvumi kwamab msanii Diamond Platnumz na msanii chini ya lebo yake ya WCB, Zuchu wanachumbiana unazidi kukolea munyu huku vielelezo na dalili zote zikiashiria hilo.

 Hii ni baada ya msanii Diamond kuonekana amevalia shati tao lenye picha ya msanii Zuchu kwa mbele huku akiwa amejiweka vizuri kwa ajili ya kupigwa picha hiyo.

Katika picha hiyo ambayo ilivujishwa na watu mbalimbali mitandaoni, Diamond anaonekana kweney shati tao hilo lenye picha ya Zuchu akiwa amevalia kikofia.

Picha hii ilizua maoni kinzani miongoni mwa mashabiki wa wasanii hao huku wengine wakidai kwamba hakuna kubwa hapo kwani ni kawaida kuvalia nguo yenye picha ya mtu ambaye ashakuwa staa mkubwa na si jambo geni kutokea kutoka kwenye fani ya michezo hadi Sanaa.

“Kawaida tu mbona hata sisi mtaani tunavaa nguo zenye picha zake na za watu wengine Kama Alikiba, Samatta, Messi, Ronaldo, na wengine wengi. Hakuna ubaya eti,” mmoja kwa jina Martina Ngoni aliandika.

Wengine walisema ndio mwanzo kabisa msanii huyo anapagawa kwenye penzi la Zuchu na ndio atazidi kuonesha viashiria vyote hadi mahasidi wakome.

“Mimi huwa nashangaa Zuchu amekuwa Wasafi muda mrefu ila Diamond hakumpenda hapo awali alimpenda Tanasha Donna lakini Zuchu sasa hivi ni staa ndio Diamond anajifanya kapagawa,” mwingine alidakia.

Hii si mara ya kwanza kwa wasanii hao kuashiria wazi kwamab huenda wanachumbiana ila wanapoulizwa hadharani huwa wanakataa katakata na kusema ni kazi tu za kimuziki.

Wiki iliyopita wakati Diamond alikuwa yupo ziarani ulaya, Zuchu alimfuata na kukutana naye kule Ufaransa ambapo haijulikani kipi kilichomchukua kule au ni kumfuata tu Diamond ambapo baadae walionekana kweney picha na video wakiwa katika mkao wa kuashiria huba kabisa.