"Mrembo alinipenda, wewe wacha domo zege!" Stevo Simple Boy amjibu Rapdon

Rapdon ni jamaa kutoka Bungoma anayedai mchumba wa Stevo Simple Boy alikuwa mchumba wake.

Muhtasari

• Rapdon alijitokeza kudai kwamba Stevo alimchukulia mpenzi wake.

• Stevo alimjibu kwamba kama mrembo alimchagua yeey na kumuacha Rapdon basi huyo jamaa afyate wake ulimi.

Image: INSTAGRAM// STIVO SIMPLE BOY

Wiki moja baada ya msanii Stevo Simple Boy kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake mpya kwa jina Gee, sasa mwanaume mmoja amejitokeza wazi kusema kwamba Gee alikuwa mchumba wake.

Mwanaume huyo kwa jina Rapdon aliandika kwenye Instagram yake akidokeza kwamba mchumba wa sasa wa Stevo Simple Boy alikuwa ni mchumba wake, huku akidhibitisha kwa kuambatanisha malalamishi hayo kwa picha yao wakiwa wamekumbatiana kabla Simpl Boy hajapindua serikali.

“Tulikuwa tunachumbiana na mchumba wa sasa wa Stevo Simple Boy,” Rapdon aliandika Instagram.

Aidha katika taarifa nyingine zilizofichuliwa na kundi moja la mitandaoni la udaku nchini, mwanaume huyo alielezea kwa kina jinsi matukio yalivyokuwa kabla ya mambo kumuendea mrama ambapo aliamka asubuhi moja tu na kukuta yule aliyekuwa akimuita mchumba wake sasa ni kama shimeji wake.

Alielezea kwamba yeye ni mwanamuziki anayechipukia na alikuwa katika mapenzi na Gee kwa takribani miezi sita ambapo asubuhi moja aliamka akapata mpenzi wake anazungumziwa mitandaoni kwamba Stevo Simple Boy amemchukulia mpenzi wake.

Baada ya madai hayo kumfikia nguli huyo wa Freshi Barida, sasa Simple Boy amejibu madai hayo na kusema kwamba mapenzi si kitu cha kulazimisha bali ni kutu kinakuja chenyewe na kusema kwamab kama Gee hakumpenda Rapdon na kumchagua yeye basi mengine ni ziada tu.

“Kama kichuna wangu hakupenda Rapdon na kunipenda mimi, hiyo basi akome, anyamaze awache kupiga mdomo zege. Mimi kwangu hizo picha na video hazileti vurugu kwa sababu kama mrembo ameshanipenda ndio hivo amenipenda, haina haja ya vita,” Stevo Simple Boy alisema.

Kwa upande wake, Gee alisema kwamba kutokana na video na picha ambazo zimekuwa zikipakiwa na mwanaume huyo, hakuna kikubwa kilichokuwa kikiendelea baina yao na kusema kwamab Rapdon ambaye anadai alikuwa mchumba wake si kweli kwani yeye alikuwa anamchukulia kama ndugu yake.

“Rapdon alikuwa kama kaka yangu na aliamua kupakia hivo nikamwambia azitoe lakini sijui ni kwa nini alikuwa ameamua kufanya hivo,” Gee alisema.