Kakake Diamond, Romy Jones aomba radhi kwa kuvujishwa picha za utupu wake

Alisema hajui nani aliyezifikisha picha hizo kwa mange Kimambi ambaye alizivujisha

Muhtasari

• RJ the DJ alisema picha hizo alizipiga wakati alikuwa mlevi na hajui zilimfikia aje Kimambi kutoka kwa simu yake.

Kakake Diamond Platnumz, Romy Jones almaarufu RJ the DJ
Kakake Diamond Platnumz, Romy Jones almaarufu RJ the DJ
Image: Instagram//Romy Jones

Kaka wa Msanii Diamond Platnumz RJ the DJ Kkwa mara ya kwanza kabisa amefunguka kuhusu Sakata la picha za utupu wake kuvujishwa mitandaoni na mwanaharakati wa kimitandao, Mange Kimambi.

RJ amechukua fursa hiyo pia kuwaomba watu haswa mashabiki wake wengi waliokwazika na kitendo kile msamaha na kusema kwamba hajui zilimfikiaje Kimambi ila anahisi ni fundi wa simu alizivujisha baada ya kumpelekea simu kuikarabati.

"Zile picha zilizovujishwa na Mangekimambi ni za Muda Mrefu nlirekodi nilikuwa Nimelewa na sijui Nani aliamua kuzivujisha Kwa Sababu Kuna Mtu alipigia simu akaniambia Nina Picha zako za Utupu ili nisizipakie Nitumie Milioni moja nizifute Mimi nikashtuka sikumtumia Pesa akaamua kumtumia huyo aliezipakia. Ile Simu niliyokuwa natumia mwanzo iliharibila halafu niliipeleka Kwa Fundi ili aitengeneze sijajua Kuwa yeye ndie aliamua kuzivujisha ama Vipi Kwa Sababu nlivyomfata kumuuliza akaniambia simu ameshaiflash" RJ the DJ alizungumza.

Aliwataka rasdhi wote kuanzia familia yake ambayo ni mke wake, ndugu zake kina Diamond Platnumz na pia mashabiki wa Wasafi yote ambako anafanya kazi kama mcheza santuri rasmi wa kakake.

"Nichukue Fursa Hii kuomba Msamaha Kwa Mungu, Mke wangu, familia yangu pamoja na Mashabiki wangu wote haijalishi yalikuwa ya kweli au ya Uongo" Kaka na Dj wa Msanii DiamondPlatnumz, RJ alisikitika.

Vile vile, msanii huyo alitumia fursa hiyo kufunguka siri za kudumu kwa ndoa yake ambayo imekuwa kwa muda mrefu ilhali ndugu yake Diamond Platnumz ameshindwa kudumisha ndoa hata miaka mitano mfululizo.

 

"Mara nyingi ndoa zinazodumu Kwa Muda Mrefu ni Zile ndoa ambazo nakwambia Diva Mimi Nataka Kukuoa, Kwa Sababu Mimi Ndio Mwanaume ninae shikilia Mahusiano yetu pia nashikilia familia yetu. Wewe ukiniambia Tuone Kwa Sababu labda Umeona Shoga zako wanaolewa au ndugu zako Wanasema Huyu Mwanaume mbona hakuoi umekaanae Muda Mrefu hapo utataka Uolewe na Mimi Kwa Sababu ya shinikizo. Mimi Mke wangu Hakuniambia Tuoane Bali Mimi Ndio nlimwambia Tuoane Kwa Sababu Mimi nlikuwa nipo Tayari na ndio maana Mpaka Sasa ndoa ipo" Dj wa Msanii Diamond Platnumz RJ the DJ.

Usiku wa kuamkia leo, Dj wa Msanii Diamond Platnumz RJ THE DJ Alichaguliwa Kuwa Dj Bora Afrika Mashariki Katika Tuzo za @aeau_awards