"Nampenda Paula, anapiga picha kali ndio maana nikampost" - Jay Melody

Jay Melody juzi kati alipakia picha yake sambamba na ya Paula na kuachia ujumbe mkali wa kudokeza huba

Muhtasari

• "Mimi naheshimu sana watu, hata Paula nampenda, namuona anapiga picha kali ndio maana nikaipakia tu,” Jay Melody alisisitiza lengo lake.

Msanii wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Jay Melody
Msanii wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Jay Melody
Image: Instagram//JayMelody

Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Jay Melody amefunguka wazi kuhusu picha ya mwanadada Paula Kajala ambayo aliipakia juzi kati kweney Instagram yake na kisha baadae kuifuta.

Akizungumza katika kipindi cha Refresh pale kituo cha habari cha Wasafi, Melody alijitetea na kusema kwamba alipakia picha mbili na wala hakuwa na maana kwamba anamutolea macho ya kimapenzi Paula bali anamkubali tu kama anavyowakubali mashabiki zake wengi tu.

“Kama utakuwa ulikuwepo makini sana utagundua kulikuwepo na picha mbili. Picha moja ni ya kwangu nimepiga na ua kichwani na ya pili ni ya Paula. Mimi nampenda kama miongoni mwa watu wengine ninavyowapenda. Namuona picha zake nzuri na ile niliyoipakia niliipenda lakini maelezo niliyofuatisha kwenye picha zile hayahusiani na picha yake,” Jay Melody aliitetea hatua yake ya kupakia picha ya Paula sambamba na yake na kuachia kapsheni ya kimahaba.

Msanii huyo alisema kwamba wala hawana ukaribu wowote  na Paula na hata hawajawahi kuwa na maongezi ya aina yoyote na pia kusema kwamba kilichomfanya kuifita ile picha ni baada ya kuona maoni ya watu na akaona haina haja kumtengenezea mazingira ya msongo wa mawazo mtoto wa watu na ndio maana akaizamisha.

“Sema tu nilivyoona yale maoni ya watu nikaona sina haja ya kumtengenezea mtoto wa watu msongo wa mawazo ndio maana nikaitoa maana pale walikuja hadi wajomba zake. Mimi naheshimu sana watu, hata Paula nampenda, namuona anapiga picha kali ndio maana nikaipakia tu,” Jay Melody alisisitiza lengo lake.

Inasemekana Paula kwa sasa ni mrembo huru baada ya penzi lao na msanii Rayvanny kuingia mchangani.

Paula ni mtoto wa kipekee wa mwanamama Kajala Fridah ambaye kwa sasa anachumbiana na msanii kutoka lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize.