"Ukiona unadaiwa, jua una akili timamu, mbinguni utakaa karibu na Yesu" - Pastor Daniel Mgogo

Mchungaji huyo alisema si vibaya kukopa ila tatizo ni yule anayegoma kurudisha deni.

Muhtasari

• "Watu wanaodaiwa mabilioni wanalala, wamakoroma, wewe laki mbili tu hulali,” mchungaji Mgogo aliwaambia waumini

Mchungaji Daniel Mgogo
Mchungaji Daniel Mgogo
Image: Facebook//PastorDanielMgogo

Mchungaji mwenye utata mwingi kutoka nchini Tanzania kutokana na kauli zake za kuchekesha na kuelimisha kwa waakti mmoja, Daniel Mgogo sasa anasema kwamba si vibaya mtu au nchi kudaiwa madeni.

Kulingana na mchungaji Mgogo, ukiona unadaiwa basi unafaa kujua fika kwamba wewe ni mtu unayejielewa mwenye akili zako timamu zilizoboreshwa na elimu uliyopata. Alisema kwamba hata Wakristu ukiona unadaiwa basi ujue Mbinguni wewe utakuwa wa kwanza kuenda na utakaribishwa kuume kwa Baba.

“Ukiona unadaiwa, ujue una akili timamu. Unakopesheka. Wengine wananiuliza, Mchungaji, nikidaiwa hivi, kwa hiyo ina maana mbinguni ninaenda? Saana, tena utakaa karibu na Yesu. Kibaya ni pale unapokopa hela, unapata, hutaki kulipa deni,” alisema mchungaji Mgogo katika kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Alienda mbele kutolea mfano nchi yake ya Tanzania ambayo wengi wa wananchi tangu rais maam Samia Suluhu kuchukua hatamu wanasema nchi hiyo imelimbikiza madeni mno.

“Tanzania ina madeni trilioni nyingi tu, lakini umemuona Mama Samia anapanda ndege, anakula bata. Mama hana shida. Kama wazungu wanatupa hela, wanajua nchi iko sawa. Unataka kujiua kwa sababu ya deni? Watu wanaodaiwa mabilioni wanalala, wamakoroma, wewe laki mbili tu hulali,” mchungaji Mgogo aliwaambia waumini wa kanisa lake.

Tatizo la malimbikizi ya madeni linazikumba nchi nyingi tu za Afruka, haswa mikopo kutoka taifa la Uchina ambayo mingi ni ya kuwekeza katika miundo msingi na miundo mbinu.

Matamshi haya ya mchungaji Mgogo yanakuja wakati ambapo nchini Kenya wananchi wanazidi kulia kwa maisha magumu huku deni la kitaifa likiongezeka kwa zaidi ya trilioni 9.