"Nimempata!" Nameless afurahia kukutana na mwanaume aliyecheza densi na mkewe 2004

Awali alikuwa amepakia kwamba anamtafuta mwanaume huyo aliyecheza densi ya kimahaba na mkewe Wahu 2004.

Muhtasari

• "Nimerudi kumtafuta huyu mtu mwenye nguo rangi ya bluu, tuzungumze!" Nameless alikuwa ameandika awali.

• Baada ya kumpata, Nameless alisema kwamba aligundua mwanaume huyo sasa huenda ni mhubiri.

Msanii Nameless na picha ya mkewe Wahu akicheza densi na mwanaume
Msanii Nameless na picha ya mkewe Wahu akicheza densi na mwanaume
Image: Facebook//Nameless

Wikendi iliyopita msanii Nameless kutoka Kenya ambayo yumo ziara ya miezi kadhaa ya muziki nchini Marekani alichekesha wanamitandao baada ya kupakia picha kutka kwa video ambayo alidai ilikuwa ya mwaka 2004 wakiwa Marekani kutumbuiza na mkewe Wahu.

Katika picha hiyo ambayo ilionesha mwanaume fulani akicheza densi ya kimahaba kwa kumtolea macho ya tamaa mkewe, Wahu ilimfanya Nameless kufanya mzaha kwamba kando na kufanya ziara ya muziki Marekani bali pia alienda kumtafuta mwanaume yule ili wapate kuzungumza kiume.

“Onyesho hili lilikuwa katika Sanfransisco mwaka wa 2004.. Nimerudi kumtafuta huyu mtu mwenye nguo rangi ya bluu, tuzungumze! Munaonaje!? Nimwambie Nini...” Nameless aliandika kwa utani.

Watu walifurika kwenye picha hiyo yenye kuchekesha na kuachia maoni mbali mbali huku wengine wakisema kipindi hicho cha 2004 Wahu alikuwa pisi kali ambalo halingeweza kuzuia mwanaume yeyote kutomkaribia kwa densi angalau kutagusana naye.

Jumanne Nameless amepakia picha ya mwanaume yule akisema kwamba hatimaye amekutana naye bado huko Marekani na lile shati tao la bluu tena na kusema kwamba kwa vile sasa wote ni watu wazima walipata kuwa na gumzo pevu la kiutu uzima.

“Kwa wanaouliza kama tulikutana na mwanamume mwenye ngozi nyepesi mwenye t-sheti la bluu ..miaka 18 baadaye, ndio!( Hawa wanaume wa sura nyeupe wametusumbua kwa muda mrefu sana) Na nadhani alikuja akiwa amevaa t-sheti ya bluu kunizushia banaa , uthubutu! Lakini sisi sote ni Wakenya wapenda amani waliokomaa kwa hiyo tulikuwa na mjadala uliokomaa kuhusu zamani, sasa na yajayo.. Yeye ni mtu mzuri anayefanya mambo mema,” Nameless aliandika.

Kilichoshangaza wengi ni pale ambapo Nameless alidokeza kwamba anadhani mwanaume huyo kwa sasa ameshaokoka na huenda ni mhubiri. Aliuliza mashabiki wake kuhusu wahubiri wenye Ngozi nyepesi kama ndio mwanzo anafaa kuwa na mashaka zaidi.

“Nafikiri sasa ni mhubiri, kwa hiyo nisiwe na wasiwasi, ama Hawa wachungaji wenye Ngozi nyepesi ndio mwanzo niwe na wasiwasi zaidi... nacheza tu,” Nameless aliandika.

Juzi, mwanao wa Kwanza alikuwa anasherehekea miaka 16 na Wakenya hawakuachwa nyuma kwa kuwasherehekea wanandoa hao ambao wanatajwa kuwa watu mashuhuri waliodumu kwenye ndoa zaidi ya miaka ishirini sasa.