(+video) Shakilla amuita Mishi Dorah 'mende'

Shakilla alisema kila kitu kwa Mishi Dorah ni kibaya na kumlinganisha na mende

Muhtasari

• Alisema Mishi Dorah wakati wake umekwisha na sasa hivi watu wanafaa kuzungumzia watu tofauti kama kila Amber Ray na wengine.

Mwanasosholaiti Shakilla kwa mara nyingine amejipata katika jungu la utashi mitandaoni baada ya kunukuliwa akisema kwamba muigizaji Mish Dorah ni kama mende tu.

Katika video ambazo imepakiwa kwenye mtandao wa Instagram, Shakilla alikuwa akizungumza na mchekeshaji Erick Omondi ambaye amekuja na muonekano mpya kabisa wa kike akijiita jina Divalicious, Shakilla alisema kwamba Mishi Dorah ni mtu aliyepitwa na wakati na watu hawafai kumzungumzia kwa wakati huu.

“Acha kuwataja mende katika kipindi hiki, Mishi Dora ni nani? Mbona unamtaja? Yeye ni kila kitu kibaya. Kila kitu kutoka kuzungumza kwake, nywele yake, kivuli chake, muonekano wake, kujipodoa kwake, vyote ni vibaya,” Shakilla anaonekana akikandia chini Mishi Dora.

Mwanasosholaiti huyo alisema kwamba Mishi Dorah kwa sasa ni kitu kilichosahaulika kwa wakati huu watu wanafaa kuzungumzia watu kama kina Amber Ray, Shakilla yeye mwenyewe, Divalicoius na watu kama hao. Alisema kwamba watu kama Dora si watu wa kuzungumziwa kwani ni sawa na mende tu.

Shakilla hakuonekana kujutia matamshi yake alipoulizwa ni kwa nini anambatiza mwanamke mwenziwe cheo kama cha mdudu anayechukiwa sana, mende.

Mishi Dora wiki chache zilizopita alijikuta akizungumziwa mitandaoni baada ya kusemekana kutiwa mbaroni katika sehemu moja ya kujivinjari alikodaiwa kula na kunywa vileo vya zaidi ya laki moja ambapo alichekwa sana alipowataka Wakenya wamsaidie kulipa ile bili.

Baada ya kukaa nyuma ya nondo kwa siku kadhaa, msamaria mwema anayesemekana kutoka Nigeria alimlipia fidia ile na kuruhusiwa kutoka jela ambapo wiki jana alizungumza kwa mara ya kwanza na kusema kwamba aliliwa na chaw asana mule ndani.