"Kuwa na madem wengi ni kama 'rehearsal' ukitafuta mwenye anaweza kuwa mke" - Octopizzo

Octopizzo alisema yeye anac watoto wengi na hawahesabu kwa sababu bado hajamaliza kuzaa.

Muhtasari

• Msanii huyo pia alifunguka kwamba amefanya harusi tatu sasa na mke wake mmoja na kusema bado amebakisha moja ile ya kizungu.

Msanii wa kuchana mistari ya muziki Octopizzo
Msanii wa kuchana mistari ya muziki Octopizzo
Image: Instagram//Octopizzo

Msanii wa kuchana mistari wa muda mrefu humu nchini Octopizzo amesema kwamab katika maisha yake amefanya harusi mara tatu na kusema kwamba lengo lake ni kufanya harusi nne, ya nne ikiwa ni ya kizungu sasa.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee ya redio humu nchini, Octopizzo alisema kwamba watu wanamuona ni kijana lakini ana mtoto wa miaka 13 ambaye anafanya mwigo wa KCPE mwaka huu.

Octopizzo aliwafyata midomo wambea wanaosema kwamba anapenda wanawake wa kizungu sana kuliko wa Kiafrika na kusema kwamba amefanya harusi tatu na Waafrika. Pia alisema kwamba tafsiri yake ya harusi ni kwamba lazima ziwe nyingi tu na kuwashauri watu kufanya harusi kila mwaka endapo watajisikia kufanya vile.

“Nulifunga ndoa mimi Disemba mwaka jana. Nimefanya harusi tatu mimi mpaka sasa hivi, bado moja. Juu nampenda mke wangu, harusi haifai kuwa moja, labda hiyo ni ya wakristu huko. Inafaa unafanya harusi kila mwaka ukitaka. Mke wako akikupatia mtoto, harusi, anakupeleka vizuri, arusi. Nimefanya ya kortini, nimefanya ya kanisa, nimefanya ya kimila, sasa nataka kufanya ya nne ya kizungu,” Octopizzo alifafanua.

Msanii huyo aizungumzia mahusiano yake na kusema kwamba amekuwa na wachumba kadha, katika kile ambacho alikitetea kama ni njia moja ya kufanya mazoezi ya kutaka kujua ni nani miongoni mwao anaweza kuwa mke wa kuishi naye.

“Nimekuwa na wachumba wengi bana, kuwa na wachumba wengi inakuwa ni kaka uko mazoezini uko shule unataka kujua ni nani anafaa. Sasa mimi baada ya kutoka kimapenzi na wanawake wengi, hatimaye nilipata mtu mwenye anaelewa uwazimu wangu,” alisema Octopizzo na kufichua kwamba harusi zote hizo amezifanya na huyo mwanamke mmoja tu.

Msanii huyo aliyechipukia kutoka mitaa ya mabanda ya Kibera alisema kwamba uwazimu wake ni kwamba aliteseka sana maisha ya mitaani na ndio maana alitafuta na kumpata mwanamke huyo mwenye anampa amani ya nafsi na pia mwenye anaweza kumwambia kitu ashtuke na kumfanya awe bora kila siku.