"Ombi langu lililojibiwa, baraka kutoka Mbinguni" Carrol Sonie amsifia mpenzi wake mpya

Wiki chache zilizopita, Sonie alitangaza kupata mchumba mpya

Muhtasari

• Sonie na Mulamwah walitengaka mwishoni mwa mwaka jana katika kile kilichofuata kuwa msururu wa kashfa za kukandiana.

Carrol Muthoni almaarufu Sonie
Carrol Muthoni almaarufu Sonie
Image: Instagram//screengrab

Muigizaji Carrol Muthoni almaarufu Sonie anazidi kuwapa taabu majasusi wa mitandaoni baada ya kupakia picha ya pamoja na mpenzi wake mpya huku akiificha sura yake kabisa watu wasipate kumtambua na kumjua.

Carrol Muthoni kwenye instastories zake Ijumaa alipakia video akiwa anakipapasa kidevu cha mwanaume huyo wake kwa mahaba huku akiwa ameficha upande wa juu wa uso na kile kilichokuwa kikionekana ni vidole vya mkono wake vikipapasa kidevu hicho chenye ndevu zilizong’aa kama pamba ya chuma inayotumika kusugua sufuria, huku akisema kwamba ni “ombi lake lililojibiwa”

Kwenye picha ya pili, Sonie alipakia picha wakiwa wamekumbatiana na mchumba huyo wake mpya kwenye kumbato na kubanana mno na kucheza wimbo wa msanii kutoka WCB Wasafi, Zuchu maneno ya “Kupendwa raha” yakisikika katika wimbo huo. Sonie anaachia ujumbe hapo akisema kwamab mwanaume huyo ni kama “Baraka kutoka juu mbinguni”

Awali Sonie alikuwa ameahidi kabisa kutoonesha sura ya mchumba wake mpya kwenye mitandao ya kijamii kwa kile alichokitaja kuwa ni funzo kubwa alilojifunza kutoka kwa mahusiano yake ya awali na mchekeshaji Mulamwah mwishoni mwa mwaka jana.

Aliwashauri mashabiki wake kwamba jijini Nairobi mtu haufai kupakia au hata kumtambulisha mchumba wako kwa wanajamii wa mitandaoni na kusema mtu utapokonywa kabla hata hujapepesa jicho.

Heh Hapana, hii Nairobi ficha mtu wako kama bangi,” Sonie alimjibu mtu mmoja aliyetaka kujua ni lini alikuwa amepanga kumtambulisha mchumba wake mpya kwa mashabiki wake mitandaoni.

Sonie na Mulamwah walitengana kwa njia chafu iliyojawa na kashfa pande zote mbili huku kila mmoja akijaribu kujitakatisha kwa kumkandia mwenzake kwamab ndiye chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano.

Pamoja na Mulamwah, walikuwa wamejaaliwa mtoto mmoja wa kike kwa jina Keilah, mtoto ambaye licha ya umri wake mchanga alijipata katikati ya zogo la wazazi wao huku kwa wakati mmoja Mulamwah akidai kwamba huenda mtoto huyo si wake na katika mahojiano tofauti akisema kwamba Sonie alikuwa na njama ya kuavya mimba ya mtoto Keilah ila hakufaulu.