logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) Lupita Afurahia Weledi Wa Babake Anyang' Nyong'o Kucheza 'Bop It'

“Tazama baba yangu akiweka rekodi ya kucheza Bop-It kwa mara ya kwanza! Baba yangu, @anyangnyongo, hufanya kila kitu kwa uangalifu, hata kucheza na familia yake

image
na Radio Jambo

Yanayojiri07 August 2022 - 13:53

Muhtasari


• Muigizaji huyo pia alimtakia kila la kheri katika kinyang'anyiro cha ugavana Kisumu kuelekea uchaguzi wa Agosti 9.

Muigizaji maarufu kote duniani kutoka Kenya Lupita Nyong’o amepasha moto mioyo ya jamii ya mtandano wa Instagram baada ya kupakia klipu ya video ambayo babake, mzee Anyang Nyong’o akicheza mcheza wa kuvuta na kufinya kwenye ala moja maarufu ijayotuiwa kucheza nyakati zisizo rasmi kwa maisha ya watu.

Lupita alifurahia kupakia video hiyo na kuwataka mashabiki wake kuangalia jinsi babake ana weledi wa hali ya juu huku akimtakia kila la kheri katika azma yake ya kushinda kipindi cha pili kama gavana wa jimbo la Kisumu.

“Tazama baba yangu akiweka rekodi ya kucheza Bop-It kwa mara ya kwanza! Baba yangu, @anyangnyongo, hufanya kila kitu kwa uangalifu, hata kucheza na familia yake. Ninajivunia kuwa naye kwenye timu yangu, na ninamtakia kila la kheri anapowania kuongoza timu katika Kaunti ya Kisumu kama Gavana kwa miaka mitano zaidi. Na kuwatakia watu wa Kenya uchaguzi wa amani na mafanikio!” Nyota huyo mshindi wa tuzo za Oscars aliandika.

Mashabiki wake kote duniani walifurahia klipu hiyo na wengine kusema kwamba hawakuamini ni babake kwa weledi alioonesha.

“Hii ni nzuri sana, niliitazama mara mbili! Kila la heri kwa baba yako. Upendo na heshima kutoka Bosnia,” shabiki mmoja kutoka Ulaya aliandika.

Muigizaji huyo Mkenya ambaye anaigiza katika filamu za Mexico alitambulika kote duniani aliposhinda tuzo maarufu duniani ya Oscars mwaka wa 2014 kama muigizaji shirikishi bora wa kike.

Hii si mara ya kwanza anaonesha urafiki na ukaribu wake na babake msomi profesa Anyang’ Nyong’o ambaye ndiye gavana wa pili wa kaunti ya Kisumu.

Lupita Nyong’o alizaliwa nchini Mexico miaka ya 80 baada ya babake ambaye kipindi hicho alikuwa mwanaharakati dhidi ya serikali dhalimu ya hayati rais Moi kuitorosha familia yake kuelekea nchi hiyo ya Amerika kusini kwa kuhofia maisha yao kutokana na uanaharakati wake dhidi ya Moi. Baada ya hali kuwa shwari, mzee Nyong’o alirudi nchini na familia yake lakini Lupita mapenzi yake ya kuigiza na mandhari ya Mexico yalimfanya kurudi kule miaka kadhaa baadae na kuanza kuigiza kwenye filamu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved