"Zuchu ni Rafiki Yangu, Huwa Tuna'chat WhatsApp Mara Kwa Mara" - Nandy

Nandy alisemqa sauti ambayo Mwijaku alivujisha ni ya uchonganishi.

Muhtasari

• “Mimi siwezi zungumzia mambo ambayo najua ni uongo kwa mtu ambaye ni muongo," Nandy alizungumzia sauti iliyovujishwa na Mwijaku.

Wasanii malkia wa bongo fleva Zuchu na Nandy
Wasanii malkia wa bongo fleva Zuchu na Nandy
Image: Instagram

Msanii Nandy amefunguka ukweli kuhusu uhusiano wake na msanii mwenziwe wa kike kutoka WCB Wasafi, Zuchu.

Katika mahojiano ya kipekee na mtangazaji Millard Ayo, Nandy alisema kwamba yeye na Zuchu ni marafiki wakubwa licha ya wengi kuwaona kama mahasimu wa kimuziki, haswa kutokana na dhana kwamba wawili hao ambao ndio wanawake pekee wanaotamba kikweli katika anga za muziki wa bongo fleva hawajawahi keti chini pamoja na kuandaa collabo.

Pia wengi walitilia mashaka hata zaidi mahusiano yao baada ya sauti kuibuka iliyosemekana kuwa ya Nandy akitoa maelekezo kwa mtangazaji Mwijaku jinsi ya kumkandia Zuchu ili asirambe dili ya kuwa balozi wa kampuni moja ya vileo nchini Tanzania.

“Zuchu ni rafiki yangu sana na huwa mara nyingi tunaadikiana jumbe kweney mtandao wa kijamii wa Whatsapp. Nilivyotoka kwenye harusi aliniandikia meseji ya kunipongeza,” Nandy alisema.

Nandy pia alipata nafasi ya kuzungumzia sauti iliyovujishwa na mwijaku ambaye alisema aliamua kuivujisha kutokana na msanii Nandy kukataa kumlipa malimbikizi yake aliyompa kazi ya kumchafulia Zuchu jina.

“Mimi siwezi zungumzia mambo ambayo najua ni uongo kwa mtu ambaye ni muongo, mimi ni afadhali nikamfichulia Zuchu kwamba ilikuwa hivi na hivi tukamalizana sisi wenyewe, kuliko nipeleke kwenye mtandao kwa sababu nina mashabiki eti sasa muone. Hakuna kitu chochote cha ukweli kwamba mimi nilitaka kumharibia mtu,” Nandy alifunguka.

Nandy alisema kwamba Mwijaku hata senti moja nyekundu hamdai kutokana kwa njia ile aliyoitumia na kumtaja kama mtu muongo tu aliyetaka kupata ufuasi mkubwa mitandaoni kwa kuona pale anapiga kuwa ndipo panaeza mfanya akatrendi kwenye mitandao ya kijamii.

Msanii huyo alizidi kusema kwamba hata baada ya uvumi huo bado wanazungumza na Zuchu na wala hawajawahi kuongelelea suala lile bali wanaongea vitu vingine tofauti kwa sababu kwamba suala kama hilo lipo wazi na hakuna ugomvi baina yao hata kidogo.

Nandy na Zuchu ndio wasanii wanaotajwa kuwa malkia wa miziki ya bongo fleva katika kizazi hiki, kuchukua usukani kutoka kwa wasanii wakongwe kama vile Ray C na Lady Jaydee miongoni mwa wengine waliotamba enzi zao.