Juliani Atangaza Kupata Mtoto wa Kiume na Lilian Ng'ang'a

Juliani alikuwa katika uhusiano wa muda mrefu na muigizaji Brenda Wairimu ambaye walipata mtoto mmoja wa kike na yeye.

Muhtasari

• Juliani alikuwa katika uhusiano wa muda mrefu na muigizaji Brenda Wairimu ambaye walipata mtoto mmoja wa kike na yeye.

Juliani na mke wake Lilian Nganga
Juliani na mke wake Lilian Nganga
Image: HISANI

Mwanamuziki wa kuchana mistari nchini Kenya Juliani na mchumba wake Lilian Ng’ang’a ambaye alikuwa mke wa gavana wa Machakos Alfred Mutua wameweka wazi kwamba ndio wazazi wapya mjini baada ya kubarikiwa na mtoto wa kiume hivi majuzi.

Akiongea na Mtangazaji ambaye pia ni mwanablogu Presenter Ali, Juliani alielezea jinsi alivyoshukuru kuwa baba tena. Pia alizungumza kuhusu uzoefu wake mpya na mwanawe akisema ilikuwa tofauti na alipokuwa akimlea binti.

"Nina watoto wawili. Msichana na mvulana. Nilimkaribisha mtoto wa kiume hivi majuzi na Lilian Ng'ang'a," alisema kwa furaha na tabasamu.

Juliani pia alisema kuwa hataki kuwaambia umma kuhusu hilo bado lakini alifurahishwa sana na hilo.

"Sikutaka kusema mengi kuhusu hilo lakini tulipata mtoto kwa hiyo mimi ni baba wa watoto wawili. Ukweli ni kama baba kwa mtoto wa kiume, hauhusiki sana." Aliongeza kusema mwanamuziki huyo aliyetambulika kwa kibao cha uanaharakati cha ‘Utawala’

Wapenzi hao walifunga ndoa ya faragha katika Paradise Lost mnamo Februari 2, 2022, mbele ya familia na marafiki wa karibu. Orodha ya wageni ilikuwa chini ya watu 50. Ilikuwa wakati huo kwamba mashabiki wake waligundua kuwa alikuwa anatarajia mtoto baada ya majasusi wa mitandaoni kuona kitumbo.

Juliani huepusha uhusiano na watoto wake na ni machache sana yanayojulikana kuhusu watoto wake. Alipomkaribisha mtoto wake wa kwanza na mwigizaji Brenda Wairimu, Juliani alikuwa akilinda sana uhusiano wake na mtoto mchanga na ni kwa mara chache sanac alionekana akipakia picha za pamoja na mtoto huyo.

Aliambia baadhi ya vyombo vya habari, "Ndio, mtoto ni wangu. Nimekuwa naye (Brenda) kwa miaka minne na tumepanga. Namshukuru Mungu, kwa hili ni baraka. Huwezi jua, tunaweza kuwa wazazi wa kiongozi mkuu."

Akiwa amebanwa zaidi, Juliani alieleza kwa nini hakuwa anapakia picha za bintiye kwenye mitandao ya kijamii.

"Lakini kwa nini tunapaswa? Kwa sababu kila mtu anafanya hivyo. Hapana, si lazima. "Watu wote wanapaswa kujua ni kwamba mtoto yuko sawa. Tunampenda na ni nzuri kumuona akikua. Mama yake pia yuko sawa. Sisi sote tuko vizuri. Kila kitu kiko sawa. Hiyo inapaswa kufupisha kila kitu unachotaka kujua juu yao. ." alisema Juliani kwa kipindi fulani.