logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Kufuatilia Kura za Kenya ni Presha, Tayari Nahisi Kujiendea Haja Kubwa" - Mtangazaji wa Uganda

“Mimi ninapofuatilia kuhesabu kura za Wakenya na shinikizo nililo nalo ni kweli kana kwamba ni Mkenya. Nadhani hata nimepata ugonjwa wa Kuhara,” - Mbabazi

image
na Radio Jambo

Habari11 August 2022 - 04:38

Muhtasari


• Mashabiki wake walizua utani mkubwa kwenye ukurasa huo wake huku wengine wakimuambia kwamba anapenda kufuatilia mambo ya Kenya kwa sababu damu yake ipo huku.

 

Mtangazaji wa Uganda, Lucy Mbabazi

Mtangazaji mwenye utata mwingi kutoka nchi Jirani ya Uganda kwa jina Lucy Mbabazi amewachekesha Wakenya kwa mara nyingine tena baada ya kupakia video akidai kwamba anafuatilia shughuli nzima ya kuhesabiwa kwa kura za urais nchini Kenya mubashara kweney runinga.

Katika video hiyo ambayo aliipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook, Mbabazi aliifuatisha kwa maneno kwamba anafuatilia kuhesabiwa kwa kura hizo huku akionekana mwenye kuhaha sana pasi na kutulia kaam mtu anayesokotwa na tumbo.

Alidokeza kwamba shinikizo la kufuatilia mchakato huo kama unavyoendelea kutoka kituo kikuu cha kuhesabu kwa kura Bomas Nairobi na shinikizo hilo tayari limeshamzushia kuendesha tumbo.

“Mimi ninapofuatilia kuhesabu kura za Wakenya na shinikizo nililo nalo ni kweli kana kwamba ni Mkenya. Nadhani hata nimepata ugonjwa wa Kuhara,” Mbabazi aliandika kwenye video hiyo.

Mashabiki wake walizua utani mkubwa kwenye ukurasa huo wake huku wengine wakimuambia kwamba anapenda kufuatilia mambo ya Kenya kwa sababu damu yake ipo huku.

Itakumbukwa hii si mara ya kwanza kwa mtangazaji huyo kuzua mjadala mkali nchini haswa wakati wa mashindano ya riadha huwa anasema baadhi ya wanariadha wa Kenya wana mizizi ya ukoo wao nchini Uganda.

“Una presha kwa sababu unawapenda sana wakenya. Huwa ninaona muda mwingi unapenda kuwazungumzia sana. Wewe mwanamke lazima uwe na damu ya Kenya,” shabiki mmoja alimwambia.

Bila shaka shughuli ya kuhesabu kura kwa amani na haki nchini Kenya ni jambo geni kwa Waganda wengi ambao wamezoea udhalimu wa rais wa muda wote Yoweri Museveni ambapo mara nyingi uchaguzi unapofanywa huwa si wa haki kwa asilimia kubwa kama mataifa mengi yenye ukomavu kidemokrasia.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved