“Kaka imetosha sasa tunajua umekutana nao wote” Ommy Dimpoz asutwa kisa kupakia picha

Ommy Dimpoz yuko ziarani nchini Uingereza

Muhtasari

• "Nawaza tu spidi uliyokuwa unatumia ya kutoka hapa kwenda pale kupata picha… na lugha sasa…”

Watanzania wamjia juu Ommy Dimpoz kisa kupakia picha na wachezaji mbali mbali Uingereza
Watanzania wamjia juu Ommy Dimpoz kisa kupakia picha na wachezaji mbali mbali Uingereza
Image: Instagram

Baada ya msanii wa bongo fleva Ommy Dimpoz kujigamba kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kuwahi kupiga picha na baadhi ya mastaa wa soka katika ligi kuu ya Uingereza, Watanzania sasa ni kama wamechoka na kitendo hicho cha kujigamba na kama walivyokosa kukaa na neno moyoni, wameamua kumtemea zake cheche kali.

Msanii Ommy Dimpoz Jumatatu usiku alikuwa miongoni mwa mashabiki waliohudhuria mechi kali kati ya miamba wa Uingereza Liverpool na watani wao wa jadi Manchester Unted katika uwanja wa kihistoria wa Old Trafford.

Baada ya mechi hiyo, Dimpoz aliwafuata wachezaji mbali mbali na kuomba picha nao ambapo amekuwa akizipakia kwa mbwembwe mno, mwanzo akianza na ile aliyochukua na nguli wa kandanda duniani Christiano Ronaldo.

Ijumaa tena msanii huyo anaendelea kuzipakia picha hizo tu ambapo ameachia moja akiwa na mshambuliaji wa Misri Mohammed Salah ambaye anakipiga Liverpool na msururu huo wa kupakia ni kama umewafika kwenye koo watu na wamempasha kwa njia zote.

“Ommy Dimpoz Kaka imetosha sasa tunajua umekutana nao wote,” shabiki wake mmoja alimwambia.

Wengine vwalimtania jinsi alivyokuwa akiwasubiria wachezaji hao na kuomba picha nao haswa kwa lugha ya kigeni ambayo wengi wanadadisi kwamba Wabongo hawana weledi wa kihivyo.

“Siku tatu unaishi uwanjani kusubiria picha. Umefanya jambo la kishujaa sana mpwa. Nawaza tu spidi uliyokuwa unatumia ya kutoka hapa kwenda pale kupata picha… na lugha sasa…” mwingine aliandika akimalizia na emoji za kucheka.

“Ulikaa geti la kuingia unaomba picha? Umekuwa omba omba ulaya,” mwingine alimjia juu Ommy na kumfanya kujibu.

“Acha makasiriko, sema nikupe connection upige picha hata ya Mayele,” Ommy alimwambia shabiki huyo kwamba aseme amuunganishe apige picha hata na mshambuliaji hatari wa timu ya Yanga ya Tanzania.

Watanzania wamjia juu Ommy Dimpoz kisa kupakia picha na wachezaji mbali mbali Uingereza
Watanzania wamjia juu Ommy Dimpoz kisa kupakia picha na wachezaji mbali mbali Uingereza
Image: Instagram