"Yule dada nilikuwa naona kwa TV sasa naamka naye kitanda kimoja, ahsante Mungu" - Harmonize

Harmonize alimshukuru Mungu kwa kumpa kila kitu ambacho amekuwa akililia ngoa tangu zamani.

Muhtasari

• "Kutoka maisha ya kuenda mtoni kuteka maji kwa dumu kwa mguu na kubeba kichwani na ukifika unafua nguo unasubiri zikauke ili uzivae tena, ila sasa nashukuru nipo katika upeo wa muziki,” - Harmonize.

mSANII hARMONIZE AMSHUKURU Mungu kwa kumletea Kajala Masanja maishani mwake
mSANII hARMONIZE AMSHUKURU Mungu kwa kumletea Kajala Masanja maishani mwake
Image: Harmonize//Instagram

Staa mmiliki wa lebo ya Konde Music Worldwide, Harmonize ni mtu mwenye kumbukumbu nyingi sana za enzi zake za utoto huku akimshukuru Mungu pia kuhusu vile vyote ambavyo amevipata katika maisha mpaka sasa.

Ijumaa kupitia instastories zake, Harmonize aliachia ujumbe mmoja mrefu na wa kugusa sana huku akisimulia jinsi alivyokuwa akienda mtoni kuteka maji kwa dumu na kubeba kichwani.

“Eeh Mungu, najua ninauliza vingi sana kila siku, ila tafadhai endeleeni kunibariki kwa kile ambacho nakihitaji. Kutoka maisha ya kuenda mtoni kuteka maji kwa dumu kwa mguu na kubeba kichwani na ukifika unafua nguo unasubiri zikauke ili uzivae tena, ila sasa nashukuru nipo katika upeo wa muziki,” Harmonize aliachia ujumbe wenye kumbukumbu za kuliza.

Pia akigusia huba lake na muigizaji mkongwe Kajala Masanja kwa kusema kwamba kitambo alikuwa anaenda kwenye banda kulipia filamu ili kumuona ila kwa sasa hivi wanaamka na yeye ndani ya kitanda kimoja, blanketi mmoja.

“Hata yule dada (Kajala) tuliyekuwa tunamlipia shilingi 100 bandani na masala ili kumuona siku ikija runinga kijijini kwetu, sasa ninaamka na yeye na ananiita Daddy, Mungu dua langu leo linaenda kwa wasio nacho kabisa,” Harmonize aliandika.

Harmonize na Kajala wanatarajia kufunga pingu za maisha hivi karibuni baada ya miezi michache iliyopita kuvishana pete za uchumba.