Baada ya video za utupu wake kuanikwa hadharani mitandoni, Irene Uwoya hakuonekana kutishiwa wala kushtuliwa na jambo kama hilo kwani yeye alitia masikio nta na kufumba macho huku maisha yake yakiendelea kama kawaida licha ya yeye kugeuka kinyago na kuzungumziwa pakubwa na watu.
Mjasiriamali huyo ambaye pia ni muigizaji wa muda mrefu sasa amedai kwamba yeye hana haja na watu wanaomtafuta kwa udi na amabri ili kumkatishia furaha yake kwani hana muda wa watu wanaolenga kumpa shinikizo lla damu hali ya kuwa hawampi pesa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Uwoya aliachia ujumbe mmoja wa kimafumbo akiwausia mashabiki wake kwamba hakuna haja ya kumruhusu mtu kukupa presha hali ya kuwa hakupi pesa kwani ukipatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu utahitaji pesa kutibiwa na pesa hizo mtu unayemruhusu kukudhoofisha hakupi.
“Kwanini unaruhusu mtu hakupi pesa akupe presha,utanunua dawa na nini!?” aliandika Irene Uwoya.
Watu wengi walioachia maoni yao walijaribu kumrushia vijembe kuhusu tukio la awali ambapo Mange Kimambi alivujisha video za utupu wake ila Uwoya katika nafasi yake kama mwanamke bomba alisimama tisti na kulikwepa kabisa suala hilo kwani ni jambo lililotokea na lieshapita na yeye hawezi kuliruhusu kumpandisha shinikizo la damu.
Uwoya akionekana kuwapuuza zaidi wale wanaotamba kwa kumtania, alipakia picha nyingine ya kumshukuru Mungu kwa kumpenda licha ya misukosuko mingi baada ya tukio la kuvujishwa kwa video zake chafu.