(+video) "Jinsi Amber Ray anaonja mahusiano akiyaacha" - Eddie Butita

Video ya Butita akiuma matunda na kuyaacha huku akisema kwamba ndio jinsi Amber Ray anaonja mahusiano akiyabwaga.

Muhtasari

• Amber Ray tangu kuachana rasmi na mfanyibiashara Jimal Rohosafi amekuwa si mtu wa kutulia na penzi la mtu mmoja

Mchekeshaji Eddie Butita amemtania mwanamitindo Amber Ray jinsi anavyobadilisha wapenzi kila uchao.

Katika video ambayo Butita aliipakia kweney ukurasa wake wa Instagram, anaonekana akiuma matunda kadhaa kama tafsiri na mwanamitindo Amber Ray kujaribu mahusiano mapya na kuyabwaga muda si mrefu.

Amber Ray tangu kuachana rasmi na mfanyibiashara Jimal Rohosafi amekuwa si mtu wa kutulia na penzi la mtu mmoja huku akiwa anaingia kwenye mahusiano baada ya siku chache anatangaza kwamba imeshindikana na mtongwe umezama baharini.

Hilo ndilo limemfanya Butita kuonyesha jinsi mama huyo wa mtoto mmoja amekuwa akionja mahusiano na kuyaacha.

Baada ya kuachana na Jimal, Amber Ray alikuja akapatana na mchezaji wa mpira wa vikapu kutoka taifa la Sierra Leone kwa jina IB Kabba ambaye walikaa naye kwenye mahusiano kwa muda mchache kabla ya kuachana ambapo mahusiano yake ya hivi punde yamekuwa na mwanaume kwa jina Kennedy Rapudo ambaye Ray wiki iliyopita alisema kwamba mahusiano hayo tayari yamevunjika hata kabla ya watu kuyafahamu zaidi.

Kando na kuingia katika mahusiano na kutoka kwa raha zake, Ray amekuwa akituhumiwa na watu wengi kwamba ana hulka ya kudandia mahusiano ya wenyewe na kuchukua wanaume wa wenyewe, jambo ambalo katika video ya uhalisia kuhusu maisha yake amabyo aliifanya Ijumaa alikataa vikali kwamba hajawahi kumuiba mwanaume wa mtu bali wanaume hao ndio wanamtafuta.

“Sipendi wanaume waliooa kama watu wanavyodai. Ni mtazamo wao. Nimetoka na wanaume wawili tu waliokuwa kwenye ndoa, wa kwanza sikujua kuwa ameoa, alikuwa akikaa nami muda mwingi na hata kunikodishia nyumba Valley Arcade na kunipangia yote kikamilifu. Wa pili alikuja na kuniambia kwamba alikuwa akipitia changamoto na alikuwa katika mchakato wa kutafuta talaka na mke wake. Tulikuwa majirani,” Ray alijitetea kwenye video hiyo aliyoipakia kwenye YouTube yake.

Amber alisema kuwa kule kuvunjwa moyo ambako amepitia kumemfanya awe makini zaidi. Aliongeza kuwa yuko tayari kuajiri mpelelezi endapo mchumba mwingine atakuja kwake ili asiingie mikononi mwa mwanamume aliyeoa.