logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Sirudi misri tena!" Chris Rock akataa mwaliko wa kufawidhi Oscars baada ya kofi la Smith

“Mcheshi Chris Rock, 57, aliambia hadhira ya kipindi cha vichekesho cha Phoenix Jumapili kwamba aliombwa kuhudhuria hafla ya mwaka ujao - lakini alikataa fursa hiyo,” - majarida yaliripoti.

image
na Radio Jambo

Habari30 August 2022 - 11:23

Muhtasari


• Will Smith alimpiga kofi kwa kufanya mzaha kuhusu mke wake, Jada Pinkett Smith, kuhusu kuonekana kama "G.I. Jane

Will Smith akimzaba kofi Chris Rock

Miezi kadhaa baada ya muigizaji Will Smith kumzaba kofi la moto mchekeshaji Chris Rock kwa kile alisema ni kumtania mkewe mbele ya macho yake wakati wa hafla ya tuzo za Oscars za mwaka huu, mchekeshaji huyo sasa anasema kuwa alifuatwa ili kushiriki katika tuzo hizo za mwaka 2023 ila alikataa.

Kulingana na jarida la Marekani, New York Post, Chris Rock alikataa mwaliko huo kwa kusema kwamab kurudi katika ukumbi wa tuzo za Oscars ni kama kurudi kwenye eneo la tukio baya.

“Mcheshi huyo mwenye umri wa miaka 57 aliambia hadhira ya kipindi cha vichekesho cha Phoenix Jumapili kwamba aliombwa kuhudhuria hafla ya mwaka ujao - lakini alikataa fursa hiyo,” New York Post waliripoti.

Majukumu yake ya uenyeji yaliyokataliwa yangekuja mwaka mmoja baada ya Will Smith, 53, kupanda jukwaani Machi 27 na kumpiga kofi kwenye Tuzo za Oscar kwa kufanya mzaha kuhusu mke wake, Jada Pinkett Smith, kuhusu kuonekana kama "G.I. Jane” kutokana na upara wake.

Tukio la Smith kumpiga kofi moja hatari lilizua gumzo kubwa mitandaoni kote duniani mwezi Machi na baadae Smith alionekana kuomba radhi kwa kitendo kile huku akijitetea kwamba alikuwa anaitetea na kuilinda familia yake huku akifichua kwamba kichekesho cha Rock kuhusu mkewe kilikuja kwake kama kejeli kutokana na hali ya afya inayomkumba Jada ambayo inasababisha kupotea kwa nywele, hali ambayo inalmazimu kunyoa upara ambao Rock alitumia kama uwanja wa kichekesho chake pasi na kujua.

"Kwa hivyo nitakuambia, Chris, nakuomba msamaha, tabia yangu haikukubalika, na mimi huwa hapa wakati wowote unapokuwa tayari kuzungumza," Smith alisema kwa huzuni inayoonekana, ila mpaka sasa Smith hajawahi kulizungumzia suala hilo hadharani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved