Mambo yanayoonyesha mwanasoshalaiti Zari Hassan ni mzazi wa kisasa wa kipekee

Mama huyo wa watoto watano anashirikiana vizuri na mzazi mwenzake Diamond katika malezi ya watoto wao.

Muhtasari

•Ni mara nyingi ambapo mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz ameonekana akijumuika na Pinto Semwanga ,19,  na Raphael  Semwanga ,16, kujivinjari pamoja na marafiki zao kwenye maeneo mbalimbali ya burudani. 

•Baada ya kutengana na marehemu Semwanga takriban miaka minane iliyopita, Zari amekuwa kwa mahusiano mengine zaidi ya tano na kwa kawaida huwa hawafichi wapenzi wake.

Mwanasoshalaiti Zari Hassan pamoja na watoto wake watano
Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Wikendi mwanasoshalaiti maarufu Zari Hassan alionyesha picha na video zake akipiga sherehe na wanawe kwenye kilabu.

Hii haikuwa mara ya kwanza kwa mama huyo wa watoto watano kuenda nje na wanawe wakubwa na kujivinjari pamoja nao.

Ni mara nyingi ambapo mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz ameonekana akijumuika na Pinto Semwanga ,19,  na Raphael  Semwanga ,16, kujivinjari pamoja na marafiki zao kwenye maeneo mbalimbali ya burudani. 

Hii ni moja tu ya viashirio vingi vinavyoonyesha kuwa mwanasoshalaiti huyo ana uhusiano wa karibu sana na watoto wake.

Kujivinjari pamoja na wanawe bila kuzingatia pengo kubwa kati ta umri wake na wao sio jambo la kawaida hasa barani Afrika.

Kando na hilo, Zari ameonekana kuwa tofauti sana na wazazi wengi wa Kiafrika kuhusu jinsi ya kusimamia mali na biashara za familia.

Mfanyibiashara huyo mwenye umri wa miaka 42 amewaaminia  kwa kiwango kikubwa wanawe wakubwa  na usimamizi wa biashara  na mali  nyingi iliyoachwa nyuma na aliyekuwa mumewe marehemu Ivan Semwanga.

Mapema mwaka huu, Zari alianzisha mchakato wa kuhamisha uongozi wa Chuo cha Brooklyn City kwa watoto wake.

Mnamo mwezi Januari, mzaliwa huyo wa Uganda alitumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza kuwa amemteua mwanawe mkubwa Pinto Ntale kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Chuo hicho.

"Mkurugenzi Mtendaji Mkuu. mafunzo, wafundishe wangali vijana, siwezi kusubiri kumwona akichukua kampuni na kusimamia fedha,” Zari alisema.

Lingine linalomtofautisha Zari na wazazi wengine ni jinsi anaendeleza ushirikiano mzuri katika malezi na mzazi mwenzake Diamond Platnumz.

Wawili hao walitengana mwaka wa 2018 lakini hilo halijawazuia kushirikiana vizuri kuwalea watoto wao Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Ushirikiano wa Diamond na Zari ni tofauti na jinsi anavyoshirikiana na wazazi wenzake wengine. Hii ni ishara kuwa mwanasoshalaiti huyo ana sifa ya kipekee ambayo huenda wapenzi wengine wa zamani wa staa huyo wa Bongo hawana

Kiashiria kingine cha jinsi mwasosholaiti huyo anaendeleza familia yake tofauti  njia za kitamaduni za Kiafrika ni jinsi ambavyo jinsi huwa haoni ugumu kutambulisha wapenzi wapya maishani mwake.

Kina mama wengi wa Kiafrika wameshindwa kujaribu mahusiano mapya baada ya kufiwa na waume zao au ndoa zao kuvunjika kwa kuhofia jinsi jamii na familia itawachukulia.

Baada ya kutengana na marehemu Semwanga takriban miaka minane iliyopita, Zari amekuwa kwa mahusiano mengine zaidi ya tano na kwa kawaida huwa hawafichi wapenzi wake.

Hata hivyo mahusiano yake hayajaonekana kuingilia uhusiano wake na wanawe. Wanawake wengi hawajaweza kufahamu siri ya kuruka kutoka kwa uhusiano mmoja hadi mwingine bila watoto wao kuathirika.