Grand P apakia picha akijivinjari na mpenziwe Eudoxie Yao, wanamitandao wazua gumzo

Mapenzi ya hawa wawili yanazungumziwa sana mitandaoni kutokana na maumbile yao yaliyotofautiana pakubwa.

Muhtasari

• “Kimbilia maisha yako Grand P,” mmoja kwa jina Paul Tenzy Aliu aliandika.

Wapenzi hao wawili wanaonekana kujivinjari katika mahaba
Grand P na Mpenzi wake Eudoxie Yao Wapenzi hao wawili wanaonekana kujivinjari katika mahaba
Image: Facebook//Grand P

Msanii mwenye umbile la mbilikimo kutoka taifa la Guinea Grand P anazidi kuhanikiza kwenye mitandao ya kijamii na mpenzi wake kutoka Ivory Coast, Eudoxie Yao.

Grand P alipakia picha wakijivinjari na  mpenziwe kwenye ufukwe huku mwanamitindo huyo mwenye umbile nene akiwa amempakata mikononi Grand P kama mtoto wake mchanga.

Grand P alionekana mdogo sana mkononi mwa Yao lakini hilo halikumzuia kufurahia mshiko.

Sosholaiti huyo wa Ivory Coast alikuwa akimshika mwanamuziki huyo kwa nyuma huku wakicheza mchezo wa kufukuzana.

Wengi wakitoa maoni yao kwenye picha hizo ambazo Grand P alizipakia kwenye Facebook, akifukuzana na mpenzi wake, walizua utani kwamba anakimbia ili asifinywe na kukosa hewa.

“Kimbilia maisha yako Grand P,” mmoja kwa jina Paul Tenzy Aliu aliandika.

“Kuwa mwangalifu ukimwangukia anaweza asipone athari ... Aina hii ya mchezo sio mzuri... Kwa sababu ni hatari wueeh,” mwingine aliandika.

Wawili hao wanazidi kukoleza huba lao miezi kadhaa baada ya kudaiwa kutengana na kisha kurudiana.

Yao alidaiwa kumtema Grand P baada ya kuonekana akijivinjari na wanawake wakati wa kipute cha kombe la taifa bingwa barani Afrika, AFCON ila baadae msanii huyo mbilikimo alinyenyekea na kuomba radhi kwa Yao na wakarudiana.

Baadhi wanasema kwamba  hamna mapenzi baina ya wawili hao  ila mwanasosholaiti huyo anamnyemelea Grand P kwa mapato na utajiri wake kimuziki tu na wengine wanahisi wawili hao wamezama kwenye dimbwi la mahaba ya kweli.

Maoni yako ni yepi kuhusu uhusiano wa binadamu hawa wawili wenye maumbile tofauti?