Nilipewa milioni ya kwanza na umri wa miaka 20, sikutumia bidii kwa kweli - Huddah Monroe

Jux alikuwa tu project kama Raila, na iliisha - Huddah Monroe.

Muhtasari

• Mwanamama huyo pia alisema kwamba hana rafiki wa karibu hata mmoja maishani mwake.

• Watu wa karibu naye ni washikadau kibiashara tu.

Huddah asema alipata milioni ya kwanza akiwa na miaka 20 bila kutumia bidii
Huddah asema alipata milioni ya kwanza akiwa na miaka 20 bila kutumia bidii
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Huddah Monroe amefichua kwamba alitengeneza shilingi milioni yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 20 tu.

Monroe alikuwa akielezea haya wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram yake alipoulizwa ni umri upi alipata milioni yake ya kwanza kabisa katika maisha yake.

Huddah ambaye kwa sasa ni milionea mkubwa kutokana na mitikasi yake ya ujasiriamali katika kuuza vipodozi alidokeza kwamba katika umri wa miaka 20, alipata milioni yake.

Kilichokuwa cha kushangaza ni jinsi alipata hiyo milioni. Alisema kwamba mazingira yenyewe ambayo aliipata milioni hiyo ni ya kutatanisha kwani alikabidhiwa na mhisani mwema tu wala si kutokana na bidi yake.

“Nilikuwa miaka 20 tu nilipopata milioni yangu ya kwanza. Kutoka kwa msamaria mwema. Sio bidi yangu kusema ukweli,” Huddah alijibu.

Mwanafasheni Huddah ambaye kwa muda mrefu amekuwa nje ya nchi alidokeza kwamba ako na wanaume mashoga wengi ambao ni rafiki zake ila humu nchini kutokana na kupotea kwake kwa muda mrefu walishapoteleana.

Huddah alikataa kwamba yeye hana rafiki wa karibu hata mmoja kwani alijifunza kwamba dunia hii usijaribu kumuamini mtu yeyote.

Alisema kwa upande wake watu wa karibu naye ni washikadau kibiashara tu na rafiki yake ni yule ambaye wote wanafaidiana kwa njia sawa.

“Usiamini mtu yeyote. Mimi nina washikadau kibiashara. Huwa nachukua urafiki kwa umakini mkubwa kama familia. Lakini wanadamu wameumbwa kwa njia tofauti kwa hiyo kuna vile sihitaji rafiki wa karibu. Kama hatufaidiana kila mmoja basi nipo vizuri nikiwa mwenyewe,” Huddah alipasua mbarika.

Akiulizwa kuhusu uhusiano wake na msanii wa Tanzania Juma Jux ambaye walionekana kuwa na ukaribu mno, Huddah alitoa jibu la utani kabisa akimfananisha na kinara wa Azimio, Raila Odinga.

“Juma Jux ako aje?”

“Kama Raila. Ilikuwa tu mradi, na iliisha,” Huddah alijibu.