Aliyekuwa mke halali wa mfanyibiashara Jimal Rohosafi, Amira amepakia video kweney ukurasa wake wa Instagram akionesha jinsi matukio yalimtendekea na kuipoteza ndoa yake na Jimal kwa mwanamitindo Amber Ray.
Katika video hiyo ambayo wengi wanakisia ni maelezo ya jinsi Amber Ray aliingilia ndoa ya Amira na Jimal na kuvunja mahusiano yao, Vibonzo viwili vya mwanaume na mwanamke vinaonekana wakichimba mgodi.
Baada ya kuchimba mgodi kwa pamoja kwa muda mrefu, wanafikia madini ambayo wanafurahia kuyatoa.
Kinachotokea baadae ni kibonzo cha tatu cha mwanamke kinaonekana kukaribia hapo na mwanaume yule badala ya kumkabidhi mwanamke huyu wa kwanza ambaye walishirikiana kuchimba mgodi, anachukua madini yale na kuyakabidhi kwa mwanamke wa pili ambaye alikuja nyuma.
Kisha wanaondoka na huyo mwanamke wa pili na madini yale na kumuacha yule wa kwanza waliyeshirikiana kuchimba mgodi naye akilia pale mgodini na majembe yote.
Amira akifuatisha maelezo hayo ya vibonzo kwenye video hiyo, alisema kwamab hiyo ndiyo hali halisi ambayo ilimtokea.
“Hiki ndicho hasa kilichonitokea, na jinsi kidakuzi kilivyovunjika. Lakini hatimaye nilitimiza malengo yangu, nikawa mwenye furaha na amani zaidi,” Amira aliandika.
Katika maelezo hayo ya vibonzo, baada ya yule mwanaume kuondoka na mwanamke wa pili na dhahabu moja, walimuacha yule wa kwanza kule mgodini ambapo bahati yake ilikuwa ni madini kadhaa yaliyobaki naye kuyachukua kwa furana.
Amira alitumia hadithi hiyo kutoa funzo kwamba baada ya wale kuondoka na fdhahabu moja wakidhani watamkomoa, kumbe walimfungulia milango ya bahati zaidi kwani walimuacha akivuna dhahabu nyingi.
“Maadili ya hadithi; endelea kuchimba na usiangalie nyuma kwani kila wakati kuna kitu kikubwa mwishoni mwa handaki,” Amira aliandika.