Nimefika miaka 35, umri wa Wababa - Trevor Ombija ajisherehekea kuzaliwa

“Rafiki wangu wa karibu sana Jane Ngoiri husema maisha ni kwa ajili ya wale wanaoishi.. - Ombija

Muhtasari

• "Asante kwa wote walionitakia heri ya siku ya kuzaliwa kwa maandishi, mtandaoni na chini ya maji. Asante na mbarikiwe,” Ombija alisema.

Mtangazaji Trevor Ombija ahserehekea miaka 35 tangu kuzaliwa
Mtangazaji Trevor Ombija ahserehekea miaka 35 tangu kuzaliwa
Image: Instagram

Mtangazaji maarufu wa runinga alinayesherehekewa Trevor Ombija amehserehekea miaka 35 tangu kuzaliwa kwake kwa kujitungia ujumbe maalumu wenye utani mwingi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ombija alijisherehekea akijitania kwamba kufika umri wa miaka 35 si kitu rahisi kwani ndio mabano halisi ya kiwango cha ‘Wababa’ neno linalotumiwa sana kuelezea wanaume wazee wenye mihela na ambao wana hulka ya kutoka kimapenzi na wasichana wadogo kiumri.

Alisema kwamab anajaribu kujifanya kutulia lakini ndani yake anajua umri huo umekwenda sana. Ombija aliwashukuru wote waliojumuika kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii kumtakia kheri njema anaposherehekea miongo mitatu na ushee tangu kuletwa duniani.

“35 ni wewe? Ni vizuri kukuona. Hivi ndivyo ninajaribu kujituliza na kuonekana mtulivu katika miaka 35 hata kama ndani kabisa najua nimefika mabano ya ‘Wababa’” Ombija alisema kwa maandishi yaliyojawa utani na mbwembwe.

“Rafiki wangu wa karibu sana Jane Ngoiri husema maisha ni kwa ajili ya wale wanaoishi.. Asante kwa wote walionitakia heri ya siku ya kuzaliwa kwa maandishi, mtandaoni na chini ya maji. Asante na mbarikiwe,” Ombija aliongeza.