Kumekucha! Zuchu aapa kumchukulia hatua jamaa aliyemkejeli yeye na mamake

Lakini nadhani kuna Muda Inabidi Ufundishe watu namna Ya kukuheshimu - Zuchu.

Muhtasari

• "Mama Hajawahi mdhihaki mtu si mgomvi na najua wazi kwa ufahamu wangu hatumjui Kabisa huyu baba,” - Zuchu.

Khadija Kopa na binti yake Zuchu
Image: HISANI

Msanii Zuchu ameonekana kughadhabishwa na video ya mwanaume mmoja ambaye alikwa anatoa ushauri kwa Diamond kumsihi kama anampenda Zuchu basi asimuache.

Katika video hiyo, mwanaume huyo anazidi kutilia chumvi kwamba Zuchu amemrithi mamake Khadija Kopa katika kila kitu, sauti hadi maumbile yake ya maziwa kubwa na kumtaka Diamond iwapo anampenda kweli asije akamchezea na kumuacha kama ilivyo hulka yake.

Mwanaume huyo anazidi kuelezea kwa kutolea ushauri kwa Diamond kwamba wanategemea mbeleni Zuchu atakuwa kama mamake katika maumbile na kila kitu.

Alisema kwamba licha ya mwanamuziki huyo amejaaliwa sauti lakini upande wa nyuma hakujaaliwa lakini wana Imani mbeleni atakuja kuupata mwili kama wa mamake na kujaa kote kote hadi pomoni.

Haya ndio huenda yakawa matamshi ambayo yalimchukiza vibaya mno Zuchu na sasa amesema yeye hajawahi tafuta heshima kwa watu.

Msanii huyo wa kike kutoka WCB Wasafi amezidi kusema kwamab tayari amezungumza na uongozi wake na kumtaka bwana mwenye video hiyo kujiweka tayari kukabiliana naye kisheria kwani ni kama alimharibia heshima yake kumfananisha na mamake na kusema nyuma hakujaaliwa.

Sijawahi kutafuta heshima kwa wanaadamu sipotezi muda na si hulka yangu .Lakini nadhani kuna Muda Inabidi Ufundishe watu namna Ya kukuheshimu .Mimi ni Binti mwenye ndugu ,Marafiki na Familia inayonizunguka lakini pengine pia Ni kioo kwa watu kadhaa .Halikadhalika mamayangu Mzazi LEGENDARY Nguli alieipa Tasnia hii Heshima kashiriki kampeni toka za Mwalimu nyerere Mpaka Raisi wetu wa sasa mpendwa Mama yetu Mama samia .Hajawahi mdhihaki mtu si mgomvi na najua wazi kwa ufahamu wangu hatumjui Kabisa huyu baba,” Zuchu aliandika kwa Ghadhabu.

Alisema sasa ni wakati wa kuvunja ukimya wake dhidi ya wale wanaomdhihaki mama yake pamoja naye mwenyewe, na ukimya wenywe utavunjwa kwa kuchukua hatua za kisheria.

“Nadhani Imefika wakati sasa Tuwe na akiba ya Maneno huu umaarufu wa kuutafuta Bila Vipaji Matokeo yake huwa si Chanya. Nipo kwenye mazungumzo na Taasisi Zinazojihusisha Na haki za Wanawake Bado natafuta muongozo sahihi Kama mpo naomba ushiriakiano wenu .Mimi si mkamilifu kweli Lakini kuongelea maumbile yangu na ya mzazi wangu Na kutudhalilisha kwa lengo la kujipatia faida ya kimitamdao,” Zuchu alionesha kuchukizwa kwake.

“Nimeongea na Manager wangu tayari tunalishughulikia hili kisheria sijapenda na sifurahishwi na dhihaka za makusudi kama hizi .BABA ULIETENGENEZA MAUDHUI HAYA UJUMBE WANGU WA WAZI UKUFIKIE NASEMA ASANTE NA TUKUTANE KWENYE MKONO WA HAKI,” aliongeza kwa ghadhabu.