logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tajiri namba moja Afrika, Aliko Dangote ahudhuria kuapishwa kwa Ruto Kasarani

Kwa sasa, Forbes inazidi kushikilia kwamba Dangote ndiye Tajiri namba moja barani Afrika akiwa na ukwasi wa kima cha trilioni 2.3 pesa za Kenya katika mwaka huu wa 2022.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri13 September 2022 - 09:24

Muhtasari


• Tajiri huyo hajawahi kufungua tawi la moja ya biashara zake nchini na kuonekana kwake Kasarani kulidokeza huenda ana uhusiano mzuri na Ruto na huenda akaingia katika soko la Kenya.

Tajiri Dangote kasarani kushuhudia kuapishwa kwa Ruto.

Tajiri namba moja wa muda wote katika bara la Afrika, Mnigeria Aliko Dangote ni miongoni mwa watu mashuhuri waliionekana katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani kushuhudia kuapishwa kwa rais wa tano William Ruto.

Katika moja ya picha zilizopakiwa kweney mitandao ya kijamii, Dangote alionekana ameketi pembezoni mwa jaji mkuu Martha Koome huku wakisubiria ujio wa Ruto kuapishwa na rasmi shughuli kuanza.

Tajiri Dangote amabaye amefungua biashara zake katika mataifa mengi ya Afrika, hajawahi fungua biashara hata moja humu nchini na katika mahojiano ya awali muda fulani nyuma alipoulizwa ni kwa nini hataki kuingia katika soko la Kenya licha ya taifa hili kuwa kitovu cha uchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki, Dangote alinukuliwa akisema kwamab baadhi ya watu wa kutoa idhini za kufanay biashara nchini walikuwa wala mlungula hatari hata kuliko nchini mwao Nigeria.

Baada ya Wakenya kuona picha hiyo ya Dangote akiwa amehudhuria hafla ya kihistoria Kenya, walifurahi na wengine kuanza kusema kwamab huenda ikawa ndio kipindi kipya kinapambazuka kwani Mkwasi huyo huenda ana uhusiano mzuri sana na Ruto na huenda akapata fursa ya kufungua biashara zake humu nchini na kuwapa Wakenya wengi kazi.

Kwa sasa, Forbes inazidi kushikilia kwamba Dangote ndiye Tajiri namba moja barani Afrika akiwa na ukwasi wa kima cha trilioni 2.3 pesa za Kenya katika mwaka huu wa 2022.

Dangote anaongoza katika wawekezaji wa hisa katika benki kuu ya Afrika kando na kuwa na kampuni ya kutengeneza saruji ambayo amefungua tawi la kiwanda chake pia nchini Tanzania miongoni mwa biashara nyingine zenye ukwasi kwa kudondosha denda.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved