Kwa jinsi ninavyompenda Harmonize, si dini tu, hata kabila nitabadilisha - Kajala

Kajala na Harmonize walivishana pete za uchumba miezi michache iliyopita na ndoa yao inatarajiwa hivi karibuni.

Muhtasari

• Ikumbukwe Harmonize ni Muislam huku Kajala kwa muda mrefu ni Mkristu.

• Kwa upande wa kabila, Harmonize anatoka jamii ya Makonde huku Kajala akitoka jamii ya Wasukuma.

Kajala asema yupo tayari kubadili hadi kabila mradi aolewe na harmonize
Kajala asema yupo tayari kubadili hadi kabila mradi aolewe na harmonize
Image: instagram

Mwigizaji mkongwe wa filamu za Bongo Fridah Kajala Masanja amezuka na jipya kwa mara nyingine tena baada ya awali kudai kwamba amempeleka mchumba wake Harmonize kwenye ibada ya kanisani.

Safari hii, Kajala amesema kwamba mapenzi yake kwa Harmonize ni makubwa sana na hayawezi kukadirika kwa mizani ya dunia hii.

Kajala amezidi kukoleza kwa kusema kwamab kwa jinsi anavyoona mapenzi yao yanazidi kukua, ako radhi kubadilisha hata kabila, si tu dini.

Ikumbukwe Harmonize ni Muislam huku Kajala kwa muda mrefu ni Mkristu piga ua na suala la kusema ako tayari kubadili kila kitu mradi kuoana na Harmonize inaonesha jinsi amemuaminia kijana Mmakonde.

“Kwa jinsi ninavyompenda si dini tu, hata kabila nitabadilisha,” Kajala alipakia meme hiyo kwenye ukurasa wake wa instastories.

Wikendi iliyopita alipakia picha za pamoja na Harmonize na kusema kwamba ilikuwa ni baada ya kutoka kanisani, jambo ambalo lilifanya wengi kuamini kwamba amefanikiwa kumbadili Harmonize kutoka Uislamu Kwenda Ukristu.

Harmonize na Kajala walivishana pete za uchumba miezi kama mitatu iliyopita katika hafla moja ya kufana mno ambapo wengi sasa wanaamini hatua inayofuata ni harusi.

Hata mshereheshaji wa katika hafla hiyo yao iliyofanyika Milimani City, MC Gara aliwahi nukuliwa akisema kwamba ndoa ya wawili hao haifai kupita mwaka huu kwani pete itaozea kidoleni.