logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nakusihi kata mizizi ya fitina, weka mzee begani - Baba Levo amwambia Ommy Dimpoz

"Pamoja na yote uliyoongea kwa uchungu sana…!! Nakusihi kata mzizi wa fitina kamata mzee wako muweke begani" - Baba Levo alishauri.

image
na Davis Ojiambo

Burudani14 September 2022 - 13:00

Muhtasari


  • • Ommy Dimpoz aliweka wazi kwamab hawezi kumtambua babake na kuwa na mapenzi naye kutokana na kwamba mzee alimtoroka akiwa mtoto.
  • • Baba Levo amemsihi kuzika ya zamani na kumkubali mzee wake kwani baba ni yule yule tu.
Baba Levo amshauri Ommy Dimpoz kumsamehe babake

Baada ya mtangazaji Mwijaku kuibua mapya kuhusu mzee aliyesemekana kuwa babake Ommy Dimpoz na Dimpoz akaja akamkataa kwamab hamjui mzee huyo, Leo asubuhi msanii huyo amefanya video moja ya uchungu sana akizungumzia sababu zilizomfanay kumkana babake.

Mzee huyo alionekana maeneo ya Sumbawanga akifanya biashara ya kuendesha bajaj na wengi walizua gumzo mitandaoni ni kwa nini mzee wa watu anachakarika vile hali ya kuwa mtoto wake Ommy Dimpoz anakula bata akitamba kwenye miji ya watu huko ughaibuni mpaka kupiga picha na mastaa wa soka wakubwa.

Kwenye video ile iliyomgharimu Dimpoz dakika nane na ushee, alisimulia jinsi matukio yalivyojitokeza mpaka kumkana babake kabisa na kukiri kwamba hana mapenzi naye hata kidogo.

Ommy Dimpoz alielezea kwamab mzee babake alimtelekeza mamake na hata majukumu yote kuyakwepa. Mzee huyo hata mamake Dimpoz alipofariki kipindi akiwa mdogo, hakuweza kufika hata msibani na wala hakuwahi kufuatilia kujua maisha ya Dimpoz yangeendeleaje baada ya msiba wa mamake.

Dimpoz kwa uchungu mno alielezea kwamba mzee alienda akaanzisha familia nyingine na yeye alilelewa na nyanya yake mpaka nyota yake katika muziki ilipokuja kung’aa. Alisisitiza kwamba hawezi kumdhamini mzee huyo na katu hana mapenzi naye.

Sakata hilo limezua maneno mengi mitandaoni ambako baadhi wamempongeza kwa hatua hiyo ya kumtelekeza mzee kwani yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumuonesha kwamba hana haja naye.

Lakini kwa upande wa pili pia, wapo wale wanaohisi kwamba Ommy anafaa kuyasahau yaliyopita na kumshika mkono mzee wake kwani mtoto akikunyea kiganja hufai kukikata bali unaosha tu na maisha yanazidi. Baba Levo ni mmoja wa wale wanaoegemea mrengo huu wa ushauri.

“Ndugu yangu @ommydimpoz pamoja na yote uliyoongea kwa uchungu sana…!! Nakusihi kata mzizi wa fitina kamata mzee wako muweke begani…!! Nunua ist mpe aendeshe uber atoke kwenye bajaji…!! Coz sababu za baba kutomuhudumia mtoto ni nyingi na zingine huwa zinasababishwa na mama zetu pia…!! Nashuri usiingilie magomvi yao play party yako kama mtoto …!!! Na mungu atakuzidishia…!!! Mama alikubeba miezi tisa tumboni..! Huwezi jua baba alikubeba miaka mingapi kwenye korodani,” Baba Levo alitoa ushauri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved