Naskia wakisema wasichana wenye nywele fupi ndio 'wife material' - Nadia Mukami

Ukitaka kufanikiwa, pate msichana mfupi mwenye nywele fupi, si maneno yangu - Nadia Mukami.

Muhtasari

• Jana Ringtone alisema wanaume mafanikio yenu yanategemea kama mwanamke wako ni mfupi na mweney nywele fupi.

Msanii Nadia Mukami asema wanawake wazuri ni wenye mitindo ya nywele fupi
Msanii Nadia Mukami asema wanawake wazuri ni wenye mitindo ya nywele fupi
Image: Instagram,Maktaba

Msanii malkia wa muziki wa kizazi kipya nchini Kenya Nadia Mukami ameonekana kumuunga mkono msanii Ringtone katika ushauri wake kwa wanaume kuoa wanawake wafupi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mukami ameonekana kufurahia suala la watu kuzungumzia wake wa marais William Ruto na rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuhusu kimo chao kulinganishwa na wanaume wao, lakini pia jinsi walivyokuwa wamenadhifisha vichwa vyao kwa kuachia nywele fupi tu.

Mukami jana alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza katika hafla ya kuapishwa kwa rais Ruto ugani Kasarani na tangu alipojifungua mtoto amekuwa akionekana kupendelea sana nywele fupi kinyume na awali alipokuwa akisuka mitindo ya kizazi kipya.

Nadia anasema kwamab kulingana na maneno ambayo amekuwa akiyasikia kwenye mitandao ya kijamii, wanawake wafupi wenye mitindo ya kuachia nywele fupi bila kusuka mitindo changamano ndio wake halali wa kutulia kwenye ndoa. Alipakia picha akiwa na mpenzi wake msanii Arrow Bwoy.

“Kwa hii mitaa ya mitandaoni naskia wakisema wasichana wafupi wenye nywele fupi ndio wife material aaaaaah eti ukitaka kufanikiwa, pate msichana mfupi mwenye nywele fupi 😁😁😁 Si mimi nimesema,” Nadia Mukami aliandika.

Jana msanii Ringtone Apoko alipakia picha ya pamoja ya familia ya kwanza iliyoondoka na familia ya kwanza mpya ambapo wake wote walionekana ni wafupi kuliko waume wao na pia wote mtindo wao wa nywele ulikuwa sawa – nywele fupi.

Msanii huyo alitumia picha hiyo kutolea ushauri kwa wanaume kwamba ukitaka kufanikiwa maishani basi kaoe mwanamke mfupi kwa kile alisema wanawake wanrefu wanaiba nyota ya mafanikio.

Awali muigizaji na mchungaji Muthee Kiengei pia naye alikoshwa na picha ya mama hao wa taifa na kuwashauri wanawake weney matatizo ya mba vichwani kwamba siri ni kuweka nywele iwe fupi ili kuzuia mba na kujikuna kila mara.