logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Siaga njugu, parachichi, ndizi na Yoghurt" Mwanafasheni atoa siri ya unene wa mapaja

“Siri ni * siaga njugu, parachichi 🥑, ndizi 🍌, na yogurt pamoja, kunywa mara mbili kwa siku na mapaja yatamwagika kumwagika" - Arwa.

image
na Davis Ojiambo

Burudani14 September 2022 - 09:44

Muhtasari


  • • “Huwa nafanya kabisa hivyo ila nilikuwa nakunywa jioni pekee. Acha sasa nianze kunywa na asubuhi nione kama nitafika hapo,” Tina Zamo alisema.
Mwanafasheni aeleza siri ya urembo wake

Shorn Arwa, mwanafasheni na mwanamitindo kwenye mtandao wa TikTok amekuja nasiri kwa kina dada wanaotaka kung’aa na kuwa na maungo makubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Arwa ametoa siri hizo huku akiwaonya wanadada hao dhidi ya matokeo yafuatayo.

Alisema kwamab ikiwa wewe ni mwanadada unayefagilia sana kuwa na umbo nene, mapaja yaliyomwagika na shepu ya kumtoa nyoka pangoni, basi ni siku chache tu unafuata maagizo yake na matokeo yanafuata.

Alisema siri ya kuwa na mapaja yaliyomwagika vizuri ni kuchanganya parachichi, ndizi, njugu miongoni mwa vitu vingine ambavyo kwa pamoja unavisaga na kunywa kwa siku chache tu.

“Siri ni * siaga njugu, parachichi 🥑, ndizi 🍌, na yogurt pamoja, kunywa mara mbili kwa siku na mapaja yatamwagika kumwagika. Shida sasa ni tumbo wadau,” Shorn Arwa alitoa ushauri kama vile daktari.

Katika klipu hiyo, Arwa alikuwa anaonekana tofauti kabisa na alivyokuwa anaonekana kwenye mtandao wa TikTok na hili lilifanya wengi kutoamini kama ni yeye huku baadhi wakisema kwamba amewacheza pengine kwa kuhariri uso wake na picha ya mtu tofauti mweney umbo kama hilo.

“Hapa tumechezwa, photoshop wewe,” muigizaji Daddie Marto aliandika huku akifuatisha kwa emoji za kucheka.

Wengine walionekana kukumbatia ushauri huo wake huku mmoja akisema kwamba alikuwa anatumia bidhaa hizo ila mara moja kwa siku na kuahidi kwamba sasa ataanza kutumia mara mbili kama vile Arwa alishauri.

“Huwa nafanya kabisa hivyo ila nilikuwa nakunywa jioni pekee. Acha sasa nianze kunywa na asubuhi nione kama nitafika hapo,” Tina Zamo alisema.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved