"Siaga njugu, parachichi, ndizi na Yoghurt" Mwanafasheni atoa siri ya unene wa mapaja

Wengine hawakuamini na kusema kwamba huenda alicheza kwa Photoshop.

Muhtasari

• “Huwa nafanya kabisa hivyo ila nilikuwa nakunywa jioni pekee. Acha sasa nianze kunywa na asubuhi nione kama nitafika hapo,” Tina Zamo alisema.

Mwanafasheni aeleza siri ya urembo wake
Shorn Arwa Mwanafasheni aeleza siri ya urembo wake
Image: instagram screengrab

Shorn Arwa, mwanafasheni na mwanamitindo kwenye mtandao wa TikTok amekuja nasiri kwa kina dada wanaotaka kung’aa na kuwa na maungo makubwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Arwa ametoa siri hizo huku akiwaonya wanadada hao dhidi ya matokeo yafuatayo.

Alisema kwamab ikiwa wewe ni mwanadada unayefagilia sana kuwa na umbo nene, mapaja yaliyomwagika na shepu ya kumtoa nyoka pangoni, basi ni siku chache tu unafuata maagizo yake na matokeo yanafuata.

Alisema siri ya kuwa na mapaja yaliyomwagika vizuri ni kuchanganya parachichi, ndizi, njugu miongoni mwa vitu vingine ambavyo kwa pamoja unavisaga na kunywa kwa siku chache tu.

“Siri ni * siaga njugu, parachichi 🥑, ndizi 🍌, na yogurt pamoja, kunywa mara mbili kwa siku na mapaja yatamwagika kumwagika. Shida sasa ni tumbo wadau,” Shorn Arwa alitoa ushauri kama vile daktari.

Katika klipu hiyo, Arwa alikuwa anaonekana tofauti kabisa na alivyokuwa anaonekana kwenye mtandao wa TikTok na hili lilifanya wengi kutoamini kama ni yeye huku baadhi wakisema kwamba amewacheza pengine kwa kuhariri uso wake na picha ya mtu tofauti mweney umbo kama hilo.

“Hapa tumechezwa, photoshop wewe,” muigizaji Daddie Marto aliandika huku akifuatisha kwa emoji za kucheka.

Wengine walionekana kukumbatia ushauri huo wake huku mmoja akisema kwamba alikuwa anatumia bidhaa hizo ila mara moja kwa siku na kuahidi kwamba sasa ataanza kutumia mara mbili kama vile Arwa alishauri.

“Huwa nafanya kabisa hivyo ila nilikuwa nakunywa jioni pekee. Acha sasa nianze kunywa na asubuhi nione kama nitafika hapo,” Tina Zamo alisema.