Mwanamitindo na mjasiriamali Hamisa Mobetto amepuuzilia mbali madai ya chawa Baba Levo kuwa msanii na bosi wake Diamond Platnumz anamrushia mkwanja mrefu kwa ajili ya matunzo ya mtoto.
Kupitia ukurasa wa Instagram, Baba Levo alifika pale na kuachia maoni hayo muda mchache tu baada ya kutoa ushauri mrefu kwa Ommy Dimpoz kumaliza tofauti zake na babake na kumkwamua kutoka hali ya umaskini.
Ommy alikuwa amedinda kabisa kutokana mtu yeyote kumuambia kuhusu babake kwa kile alisema mzee alimtelekeza na Baba Levo alimtaka kumsaidia mzee wake japo kumsaidia ili aondokee umaskini.
Baba Levo alimtania Hamisa Mobeto kwamba naye asije akasema Diamond hamshughulikii mwanawe, jambo ambalo Mobetto alikanusha vikali na kusema mwanawe anamtegemea katika kila kitu na Diamond hajawahi toa hata senti.
“Kwako Ushahidi tunao Tajiri anamwaga mahelaaaa,” Baba Levo aliandika.
“Tajiri gani kwanza tuanzie hapo? Anazimwaga wapi huenda nikakusaidia tukaenda kuziokota,” Hamisa Mobetto alijibu.
“Basi mama, huenda kweli hatoi chochote,” Baba Levo alitania.
Wiki kadhaa zilizopita katika mahojiano na wanablogu, Hamisa Mobetto alisema Diamond alimtelekeza mtoto wake na hata siku ya kusherehekea kuzaliwa kwake, msanii huyo hakusema chochote cha kumtakia heri.
Mobetto alionekana kutotaka kuzungumzia suala lolote linalomhusu Diamond katika kile kilionekana kuwa katika siku za hivi karibuni wawili hao hawana ushirikiano mwema katika malezi ya mwanao.
Diamond akiwa Ujerumani aliwahi nukuliwa akitamba kwamba yeye huwa anawashughulia wanawe wote licha ya kutengana na kina mama zao.