Saini ombi la kutaka barabara moja South C kuitwa E-Sir - Nameless awarai Watu

Miaka 19 iliyopita, Kenya ilipoteza hazina ya kitaifa, E-sir.

Muhtasari

• Kwa heshima ya msanii huyu mashuhuri wa Kenya tunatoa wito kwa barabara ya South C ipewe jina lake - Muthoni Maingi

Nameless awataka watu kutia saini ombi la kubadilishwa kwa barabara moja jina na kuitwa E-Sir
Nameless awataka watu kutia saini ombi la kubadilishwa kwa barabara moja jina na kuitwa E-Sir
Image: YouTube screengrab

Msanii mkongwe wa miziki ya kizazi kipya nchini Kenya Nameless amewasihi wakenya kutia Saini ombi la kutaka kuishrutisha serikali kuipa barabara moja katika mtaa wa South C jijini Nairobi jina la msanii waliyekuwa wanaimba naye kabla ya kifo chake miaka 19 iliyopita, E-Sir.

Kupitia instastories zake, Nameless alipakia ujumbe wa kundi la Change.org linalowataka watu wengi kujitokeza na kutia Saini ombi hilo ili serikali kumpa E-Sir heshima anazostahili kupitia kupatia barabara jina lake.

nameless e-sir
nameless e-sir

Itakumbukwa kabla ya kifo chake, E-Sir alikuwa ni mkaazi wa maeneo ya South C na mpaka kifo chake, walikuwa na msanii Nameless katika gari moja wakirejea Nairobi kutoka jiji la Nakuru mwaka 2003 ambapo walipata ajali ila kwa mapenzi ya Mungu Nameless akasalimika.

"Miaka 19 iliyopita, Kenya ilipoteza hazina ya kitaifa, E-sir. Kwa heshima ya msanii huyu mashuhuri wa Kenya tunatoa wito kwa barabara ya South C ipewe jina lake, kama njia ya kusherehekea talanta ya kisanii na kwa heshima ya kumbukumbu yake,” Muthoni Maingi aliandika kwenye Tweeter huku akimtaja Nameless ambaye pia aliupakia ujumbe huu kwenye Instastory yake.

Inaarifiwa kwamba watu wengi wameshasaini ombi hilo wakimtaka gavana mpya wa Nairobi Johnson Sakaja kusukuma barabara moja katika mtaa huo kupewa jina la nyota huyo aliyefariki angali mchanga.