Aslay amaliza ugomvi wake na Mbosso, afanya cover ya 'Nadekezwa'

Aslay na Mbosso walikuwa katika kikundi kimoja cha Yamoto Band kabla ya kundi hilo kusambaratika.

Muhtasari

• Ugomvi wao ulianza baada ya Aslay kumunfollow Instagram Mbosso na kuanza kukunjiana katika chochoro zote.

Mbosso, Aslay
Mbosso, Aslay
Image: INSTAGRAM

Miaka kadhaa iliyopita kuliibuka kundi moja la vijana wanne kutokea Tanzania kwa jina Yamoto Band. Lilikuwa ni kundi moja lenye matumaini makubwa kwenye tasnia ya bongo fleva ila baada ya kupata umaarufu kundi hilo liligawanyika na kila mmoja kuamua kujishughulisha na hamsini zake.

Baadae kuliibuka madai kwamba wasanii hao Aslay, Mbosso, Enock Bella na Beka Flavour walivunja kundi hilo kutokana na kutolewana na wengine wakasema kwamab ni tofuait za kutoafikiana jinsi ya kushea mapato.

Msanii Mbosso kwa bahati nzuri alipata mwanya akasainiwa katika lebo kubwa kabisa ya WCB Wasafi huku Aslay na Beka Flavour wakikipiga kama wasanii huru.

Aslay baada ya muda alitoweka kwenye gemu na madai yakaibuka kwamba walikuja wakakosana na Mbosso kutokana na kuoneana gere ya mafanikio.

Mbosso katika mahojiano na kipindi cha Refresh cha redio ya Wasafi alinukuliwa akisema kwamba kweli kuna tofauti kati yake na Aslay ila akadinda kuzizungumzia.

Jana Aslay baada ya kimya kirefu kwenye muziki aliibuka na mapya kwa kupakia klipu kweney Instastories zake akiimba wimbo wa Mbosso, Nadekezwa.

Hili lilitafsiriwa na wengi kuwa huenda wamepiga pasi tofauti zao na kulainisha mambo na Mbosso na huenda hivi karibuni tukamuona Aslay amerudi kwenye muziki kwa hisani ya Mbosso.

Mbosso na Aslay walifika katika hatua mbaya sana mpaka kila mmoja akaamua kum unfollow mwenzake kweney mitandao ya kijamii, Mbosso akisema kwamba Aslay ndiye alikuwa wa kwanza kuchukua hatua hiyo naye akaona hakuja haja ndio akajibu mipigo pia ya kutomfuata kule Instagram.

Msanii huyo wa Wasafi kwa kipindi cha mida mrefu amekuwa akionesha ukaribu wake na wasanii wenzake Enock Bella na Beka Flavour ila likija suala la Aslay ni kama swara na Chui kwani hawaonani kabisa.

Hivi karibuni katika tamasha la Wasafi Bet kule Morogoro, Mbosso alipanda jukwaani na msanii Enock Bell na wakatumbuiza kibao kimoja kutoka kundi la Yamoto Band.

Hatua ya Aslay kufanya klipu ya ngoma ya Mbosso kimetafsiriwa kama kutangaza amani na kudhihirisha kumalizika kwa tofauti kati yao.